Ufaransa yadai kuwa wavamizi hawatumii silaha zake katika jinai zao Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47824-ufaransa_yadai_kuwa_wavamizi_hawatumii_silaha_zake_katika_jinai_zao_yemen
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amedai kuwa, silaha za Ufaransa zilizouziwa Saudia na Imarati sizo zinazotumika kufanya mauaji ya raia nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2018 02:56 UTC
  • Ufaransa yadai kuwa wavamizi hawatumii silaha zake katika jinai zao Yemen

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amedai kuwa, silaha za Ufaransa zilizouziwa Saudia na Imarati sizo zinazotumika kufanya mauaji ya raia nchini Yemen.

Shirika la habari la AFP limemnukuu Florence Parly akielezea kusikitishwa kwake na jinai zinazofanyika nchini Yemen na kudai kuwa, silaha za Ufaransa sizo zinazotumika kuulia raia huko Yemen.

Waziri huyo wa ulinzi wa Ufaransa sambamba na kukiri kuziuzia silaha nchi vamizi za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu amesema kuwa, nchi yake haijaiuzia Yemen silaha yoyote ile.

Pia amedai kuwa, Saudi Arabia inatumia silaha inazouziwa na Ufaransa kwa ajili ya kujilinda na si katika jinai zake dhidi ya raia huko Yemen.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly

 

Muungano vamizi wa nchi za Kiarabu zinazoongozwa na Saudia kwa baraka kamili za nchi za Magharibi unafanya ukandamizaji na jinai za kutisha dhidi ya wananchi wa Yemen tangu mwezi Machi 2015 huku zikiwa zimeizingira nchi hiyo ya Kiislamu kutokea angani, baharini na ardhini.

Hadi hivi sasa vita hivyo vilivyoanzishwa na Saudia dhidi ya Yemen vimeshaua watu 14 elfu na kujeruhiwa makumi ya maelefu na kuwafanya wakimbizi mamilioni ya wengine.

Mara kwa mara taasisi za kimataifa na mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakizilaumu nchi za Magharibi ikiwemo Ufaransa kwa kuziuzia silaha nchi hizo vamizi ambazo zinazitumika kufanya jinai na kuulia watu wasio na hatia nchini Yemen.