Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametilia mkazo kuanzishwa utaratibu wa kutumia sarafu ya Riyali na Rupia katika mabadilishano ya kibiashara na kiuchumi kati ya Iran na India.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema, kushambuliwa Waislamu wakati wa tamasha la Wahindu la Ram Navami ni 'dhihirisho la wazi la kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu' nchini India.
Wanaharakati kwenye majukwaa ya mawasiliano ya kijamiii ya India wamechapisha picha zinazoonyesha shule ya Kiislamu ikiteketea kwa moto katika jimbo la Bihar, baada ya kushambuliwa na Wahindu wenye msimamo mkali siku ya Ijumaa, na kusababisha uharibifu mkubwa.
Serikali ya India imebomoa msikiti mwingine katika jimbo la Uttar Pradesh kwa kisingizio cha ujenzi wa barabara.
Ukoloni wa Uingereza ulikuwa sababu ya vifo vya zaidi ya watu milioni mia moja nchini India.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amemwita waziri mkuu wa India Narednra Modi "Chinjachinja wa Gujarat" baada ya waziri mwenzake wa India kuishutumu Pakistan kuwa "kitovu cha ugaidi" huku majirani hao wenye silaha za nyuklia wakikabiliana kwa vita vya maneno katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia jana Ijumaa alisisitiza kuwa kuna umuhimu Moscow kushirikiana na Tehran, Beijing, Ankara, New Delhi na nchi nyingine za pambizoni mwa bahari ya Kaspi.
Rais Xi Jinping wa China amesema Taiwan kuwa nchi huru na kupatikana amani katika Mlango-Bahari wa kisiwa hicho havitangamani kama yalivyo maji na moto.
Shirika la Intelijensia la Qatar limewakamata maafisa wanane wa zamani wa Jeshi la Wanamaji wa India nchini Qatar wanaoshukiwa kufanya ujasusi kwa manufaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Shughuli za uokoaji zinaendelea katika mji wa Morbi katika jimbo la Gujarat nchini India ambako watu wasiopungua 141 wameaga dunia hadi sasa baada ya daraja la enzi za ukoloni kuporomoka jana jioni.