-
Mahakama Kuu ya India na mtihani mgumu wa kutekeleza sheria au kuchagua misimamo ya kuchupa mipaka
Feb 13, 2022 00:46Kushadidi kwa mizozo na hitilafu juu ya vazi la hijabu la wasichana na wanawake wa Kiislamu katika vyuo na taasisi za elimu katika jimbo la Karnataka huko kusini mwa India kumezusha hali ya wasiwasi na hofu kwa jamii za Waislamu nchini humo.
-
HRW yakosoa marufuku ya vazi la hijabu nchini India
Feb 11, 2022 23:29Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa marufuku ya vazi la hijab inakiuka wajibu wa India chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, ambayo inadhamini haki ya uhuru wa imani ya kidini ya mtu binafsi na uhuru wa kujieleza na kupata elimu bila ubaguzi.
-
Wimbi la hasira laibuka India baada ya mwanafunzi kubughudhiwa na wahuni kwa kuvaa hijabu
Feb 09, 2022 09:53Video iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter ikimuonyesha mwanafunzi Muislamu aliyevaa hijabu akibughudhiwa kwa maneno na genge la wahindu wenye misimamo ya kufurutu mpaka katika chuo kimoja cha jimbo la Karnataka nchini India, imezusha moto wa hasira na kuzidisha malalamiko ya kupinga marufuku ya uvaaji hijabu iliyowekwa katika taasisi za elimu za jimbo hilo.
-
Chuo kingine India chazuia wanafunzi Waislamu kuvaa Hijabu
Feb 05, 2022 01:06Katika kile kinachoonekana ni kuendelea kuendekeza misimamo ya chuki na kufurutu ada ya serikali ya waziri mkuu wa India Narendra Modi, wanafunzi Waislamu wanaovaa hijabu wamepigwa marufuku kuingia madarasani katika chuo kimoja katika jimbo la Karnataka, kusini mwa India.
-
Wanafunzi Waislamu wapigwa marufuku kuvaa Hijabu katika chuo cha serikali India
Jan 21, 2022 09:49Wanachuo Waislamu wanaovaa hijabu wamepigwa marufuku kuingia madarasani katika chuo cha serikali cha Udupi kilichoko kwenye jimbo la Karnataka kusini-magharibi ya India.
-
Wito wa Wahindu wa kutekelezwa mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu waibua hasira
Dec 25, 2021 01:02Video zinazowaonyesha viongozi wa kidini wa Kihindu nchini India wakitoa wito wa mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu zimezua hasira na wito madai ya kuchukuliwa hatua dhidi ya wahusika.
-
India yawapatia uraia wasio Waislamu kutoka Afghanistan, Pakistan na Bangladesh
Dec 23, 2021 04:38Serikali ya India imesema imewapatia uraia watu elfu tatu, ambao ni raia wa jamii za wachache katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Bangladesh.
-
Waziri Mkuu wa Pakistan aionya India: Tutajibu mapigo kwa hatua ya kijeshi kama tulivyofanya 2019
Dec 18, 2021 04:11Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameionya India kuwa, endapo itajaribu kuchukua hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Pakistan, nchi hiyo itajibu mapigo kama ilivyofanya mwaka 2019.
-
Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya India na mke wake waaga dunia katika ajali ya helikopta
Dec 08, 2021 10:51Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya India Jenerali Bipin Rawat, mkewe, na watu wengine 11 wameufariki dunia baada ya helikopta ya kijeshi waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika jimbo la kusini la Tamil Nadu.
-
Shule zafungwa Delhi, India kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa
Nov 17, 2021 23:26Shule zote katika mji mkuu wa India, New Delhi zimefungwa kutokana na hali chafu ya hewa.