-
Pezeshkian awataka Wairani kuwa macho mkabala wa njama za maadui
Jan 23, 2025 04:18Rais wa Iran amesisitiza haja ya kudumisha umoja wa kitaifa nchini, wakati huu ambapo maadui wa taifa hili wanakula njama na kutaka kutumia vibaya mizozo ya ndani.
-
Zarif: Iran sio tishio la usalama kwa nchi yoyote ile
Jan 23, 2025 04:07Makamu wa Rais katika Masuala ya Kistratejia wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema Jamhuri ya Kiislamu si tishio la usalama kwa nchi yoyote ile duniani, akisisitiza kwamba kama Tehran ingelikusudia kutengeneza silaha za nyuklia, ingelikuwa imefanya hivyo zamani.
-
Iran: Tuko tayari kuanzisha upya mazungumzo ya kuondoa vikwazo
Jan 21, 2025 23:20Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisheria, Kazem Gharibabadi amesema kuna misingi na fursa zinazofaa za kuanzisha tena mazungumzo na pande nyingine.
-
Iran yasisitiza kuwa uwezo wake wa kiulinzi na kijeshi hauwezi katu kuwa suala la kujadiliwa
Jan 20, 2025 23:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amesema, uwezo wa kiulinzi wa Iran hauwezi katu kuwa suala la kujadiliwa na kuzungumziwa.
-
Kutekelezwa Makubaliano ya Kifedha kati ya Iran na Russia
Jan 20, 2025 23:03Gavana wa Benki Kuu ya Iran, Mohammadreza Farzin, amesema kuwa kupitia utekelezaji wa makubaliano ya kifedha kati ya Iran na Russia, sarafu za mataifa haya mawili zitakuwa msingi wa biashara kati ya nchi hizo kwa mujibu wa kiwango cha mabadilishano kilichokubaliwa sokoni.
-
Rais wa Iran awapongeza wananchi wa Gaza kwa ushindi dhidi ya Israel
Jan 20, 2025 07:57Rais Masoud Pezeshkian wa Iran leo Jumatatu amewapongeza wananchi wa Ukanda wa Gaza kwa ushindi wao katika kukabiliana na vita vya kikatili na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel yaliyoendelea kwa miezi 15.
-
Pezeshkian: Hatuhitaji Magharibi kulinda usalama wa eneo hili
Jan 19, 2025 02:44Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Russia kwa kushirikiana vizuri zinaweza kufuata sera huru na kudhamini usalama wa kisiasa na kiuchumi wa eneo hili.
-
Mashauriano ya Iran na Ethiopia ya kupanua uhusiano wa kiuchumi
Jan 19, 2025 02:32Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Bunge amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mshauri katika Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Ethiopia ambapo wamejadiliana njia za kupanua ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili ikiwemo uanachama katika kundi la "BRICS".
-
Araqchi: Asili ya makubaliano ya Iran na Russia ni ya kiuchumi
Jan 18, 2025 07:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya kina ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Iran na Russia yanahusu vipengee vyote vya uhusiano wa nchi na kwamba asili ya makubaliano hayo zaidi ni katika uga wa uchumi.
-
Qalibaf: Iran imesimama imara kuwatetea Waislamu duniani
Jan 17, 2025 23:12Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: Iran siku zote inasisima imara na imeonyesha kuwa ni nchi pekee inayowatetea Waislamu wote bila ya kujali madhehebu zao na imetoa maelfu ya mashahidi katika njia hii.