Wairani waadhimisha Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari
Sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari wa Dunia ambayo huadhimishwa tarehe 13 Aban (Novemba 3 au 4) kila mwaka hapa Iran, zinaendelea mjini Tehran na katika miji mingine kote Iran.
Mikusanyiko, matembezi na maandamano ya kupinga ubeberu wa dunia yanaendelea mjini Tehran licha ya baridi na mvua; na vile vile katika miji mingine ya Iran.
Wananchi wa Iran wanaadhimisha siku hii ambayo pia inajulikana kama Siku ya Wanafunzi, ikiwa ni kumbukumbu ya kutwaliwa Pango la Ujasusi (uliokuwa ubalozi wa Marekani nchini Iran).
Aban 13 ni Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu wa Dunia hapa nchini Iran, ambapo Wairani hukusanyika kuadhimisha matukio matatu makuu ya kihistoria.
Matukio hayo matatu muhimu ya kumbukumbu ni siku aliyobaidishwa na kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki Imam Khomeini (MA) tarehe 4 Novemba 1964, siku waliyouliwa wanafunzi na askari wa utawala wa Pahlavi Novemba 4, 1978 na siku ilipofanyika harakati ya kimapinduzi ya kuliteka Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran.
Miaka 46 iliyopita na katika siku kama ya leo, yaani tarehe 13 Aban mwaka 1357 Hijria Shamsia (sawa na Novemba 4, 1979), kulifanyika maandamano makubwa ya wanafunzi na wanachuo mjini Tehran, kulalamikia njama kadhaa wa kadhaa zilizokuwa zikifanywa na Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Maandamano hayo ya yalikandamizwa vibaya na askari wa utawala wa Shah na kusababisha umwagaji damu mkubwa.