Iran na Sudan zasisitiza kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara
(last modified Fri, 08 Nov 2024 02:37:28 GMT )
Nov 08, 2024 02:37 UTC
  • Iran na Sudan zasisitiza kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara

Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran na Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi wa Sudan wamekutana na kujadili upanuzi wa uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.

Katika kikao chake na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Sudan, Gibril Ibrahim Mohamed, ambaye yuko Tehran akiongoza ujumbe wa kiuchumi wa serikali ya Khartoum, Waziri wa Masuala ya Uchumi na Fedha wa Iran, Abdolnaser Hemmati ameeleza matumaini yake kuwa mahusiano ya kiuchumi na biashara kati ya Iran na Sudan yatapanuliwa zaidi katika duru mpya ya uhusiano wa nchi hizo mbili.

Mawaziri Hemmati na Gibril Ibrahim

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi wa Sudan metaja faida kama vile kuwepo kwa ardhi yenye rutuba nchini Sudan kwa ajili ya mazao ya kilimo, ikiwa ni pamoja na mbegu za mafuta, ufuta, karanga, pamoja na ufugaji na rasilimali nyingi za chini ya ardhi kuwa vinaifanya Sudan kuwa mojawapo ya fursa za uwekezaji. Gibril Ibrahim Mohamed pia ameeleza hamu ya serikali na watu wa Sudan ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Inafaa kuashiria kuwa Jamhuri ya Sudan ina eneo la kilomita za mraba 1,886,000 na idadi ya watu milioni 45. Zaidi ya 97% ya watu wa Sudan ni Waislamu.

Tags