Iran yatoa pigo kubwa la kihistoria kwa Israel
Shirika la habari la IRIB limenukuu duru za kuaminikia katika eneo hili la Asia Magharibi zikisema kuwa, taasisi ya kiintelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa pigo kubwa kwa Israel. Imefanikiwa kuhamisha kutoka kwa utawala wa Kizayuni taarifa za siri za kijasusi, nyeti na za kiistratijia ikiwemo miradi na taasisi za atomiki za Israel.
Katika upande mwingine, televisheni ya Al Alam imetangaza kkuwa, duru moja ya kuaminika imeliambia shirika la habari la Tasnim kuhusu pigo hilo kubwa la kihistoria la kiintelijensia ambalo Iran imeipiga Israel kwamba, mafanikio hayo makubwa ya kiusalama yamefanywa na watu waliokuwemo ndani ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, na ni kazi iliyofanyika kwa umakini mkubwa wa kiusalama. Maafisa usalama wa Iran wamefanikiwa kufika kwenye maeneo nyeti ya utawala wa Kizayuni na kuchota taarifa hizo muhimu mno na kuzihamishia ndani ya Iran.
Duru hiyo imeongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa imo katika kuzipanga kwenye mafungu maalumu taarifa hizo na siku za usoni itatoa ufafanuzi zaidi. Lakini kilicho wazi ni kwamba shirika la ujasusi la Israel MOSSAD halikueza kuwagundua maafisa hao wa usalama wa Iran.
Duru hiyo ya kuaminika imemalizia kwa kusema kuwa, hivi sasa Iran ina data na taarifa za kiusalama za makamanda wote wa ngazi za juu wa kijeshi na maafisa usalama wa MOSSAD.