-
Raisi aondoka Kampala kuelekea ziarani Harare
Jul 13, 2023 04:40Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Alhamisi ameondoka Kampala na kuelekea Harake mji mkuu wa Zimbabwe baada ya kukamilisha ziara huko Uganda.
-
Kanani: Visiwa vya Bu Musa, Tombu Ndogo na Tombu Kubwa ni milki ya Iran
Jul 11, 2023 23:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepinga taarifa ya pamoja iliyotolewa na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na Russia kuhusu visiwa vitatu vya Iran vya Bu Musa, Tombu Ndogo na Tombu Kubwa na kusema: Visiwa hivyo vitatu daima vitasalia kuwa milki ya Iran.
-
Kukiri Marekani kwamba hakuna mpango wa nyuklia wa kijeshi unaoendeshwa ndani ya Iran
Jul 11, 2023 23:04Licha ya madai ya mara kwa mara ya nchi za Magharibi hususan Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwamba Iran inafanya juhudi za kujipatia silaha za nyuklia, taasisi kuu ya intelijensia ya Marekani imeikiri kuwa Iran haijihusishi na uundaji wa silaha za nyuklia.
-
Magazeti ya Afrika Mashariki yaakisi safari ya Rais wa Iran katika nchi za Afrika
Jul 11, 2023 04:50Magazeti na vyombo vingine vya habari vya nchi za Afrika Mashariki vimeakisi kwa mapana safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye leo Jumanne anatazamiwa kuondoka nchini kuelekea barani Afrika kwa ziara ya siku tatu ya kuzitembelea nchi za Kenya, Uganda na Zimbabwe.
-
Helikopta za Iran ndizo zenye uwezo mkubwa zaidi Asia Magharibi
Jul 09, 2023 07:34Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Nchi Kavu la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inamiliki helikopta nyingi zaidi, za kisasa na zenye uwezo mkubwa zaidi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Umoja wa Mataifa wataka kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jul 08, 2023 23:08Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Kisiasa, amehutubia kikao cha Baraza la Usalama cha kukagua utekelezwaji wa azimio nambari 2231, na kuelezea kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ndio chaguo bora zaidi la kuhakikisha "hali ya amani ya mpango wa nyuklia wa Iran."
-
Abdollahian: Uhusiano wa Iran na Algeria upo katika mkondo sahihi
Jul 08, 2023 09:01Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari hapa Tehran akiwa pamoja na mwenzake wa Algeria Ahmed Attaf kuwa uhusiano wa Iran na Algeria upo katika mkondo sahihi.
-
NAM yatoa wito wa kufanywa juhudi zaidi kimataifa kuhakikisha Wapalestina wanarejeshewa haki zao
Jul 07, 2023 23:54Mawaziri wa mambo ya nje wa Vuguvugu la Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM, wameeleza katika taarifa ya mwisho ya kikao chao kilichofanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, Baku kwamba kuna haja ya kufanyika juhudi zaidi kimataifa za kutafuta njia ya ufumbuzi wa kiuadilifu utakaohakikisha Wapalestina wanarejeshewa haki zao.
-
Ripoti yenye malengo maalumu ya Baraza la Haki za Kibinadamu dhidi ya Iran sambamba na ghasia za Ufaransa
Jul 07, 2023 04:07Kamati eti ya kutafuta ukweli iliyoundwa na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu Iran imetoa ripoti yake ya awali kuhusu kile ilichokiita 'ukandamizaji wa Iran dhidi ya maandamano ya nchi nzima'.
-
Iran na Sudan kufufua uhusiano wao wa kidiplomasia karibuni
Jul 06, 2023 23:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Sudan kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba, ambapo wamekubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia wa nchio mbili hizi karibuni hivi.