-
Matamshi ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia dhidi ya makundi ya muqawama Asia Magharibi
Nov 02, 2021 08:53Faisal bin Farhan al-Saud, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia amesema katika mahojiano na Kanali ya Televisheni ya al-Arabiya kwamba, matatizo na mvutano wa nchi yake na Lebanon ni zaidi ya matamshi ya waziri wa habari wa nchi hiyo, kwani Saudia haikubaliani kabisa na suala la kupata nguvu waitifaki wa Iran nchini Lebanon na katika eneo la Asia Magharibi kwa ujumla.
-
Khatibzadeh: Hakuna mawasiliano ya aina yoyote baina ya Iran na Marekani
Nov 01, 2021 11:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amekadhibisha madai ya kuwepo mawasiliano baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekkani.
-
Iran yalaani kimya cha ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu vikwazo vya Marekani
Nov 01, 2021 01:19Kazim Gharibabadi Katibu Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Iran amemkosoa Javdi Rehman Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Hali ya Haki za Binadamu nchini Iran kutokana na kimya chake mkabala wa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.
-
"IAEA ipo katika mashinikizo ya Marekani na utawala wa Kizayuni"
Oct 31, 2021 23:38Mkuu wa Kamati ya Nishati ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) upo chini ya mashinikizo makubwa ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wanachuo wa Iran waunga mkono kauli ya waziri wa Lebanon dhidi ya Saudia
Oct 31, 2021 23:37Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametangaza kuunga mkono matamshi ya Waziri wa Habari wa Lebanon, George Kordahi ya kulaani mashambulio ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen.
-
Iran, Russia zasisitiza mazungumzo ya JCPOA yatafanikiwa Iran ikiondolewa vikwazo
Oct 29, 2021 23:57Iran na Russia zimesisitiza kwamba mazungumzo ya pande zilizosalia katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015 yatafanikiwa tu iwapo yatapelekea kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran sambamba na pande zote kutekeleza mapatano hayo.
-
Uhusiano wa kiuchumi wa Iran na Saudi Arabia waanza rasmi, meli ya kwanza ya Iran yatia nanga Saudia
Oct 28, 2021 03:55Mkuu wa Shirikisho la Usafirishaji Nje Bidhaa za Iran amesema kuwa, uhusiano wa kiuchumi wa nchi yake na Saudi Arabia umeanza rasmi baada ya meli moja yenye bidhaa za Iran kutia nanga katika moja ya bandari za Saudia.
-
Rais Ebrahim Raisi alaani hujuma ya kimtandao dhidi ya vituo vya mafuta vya Iran
Oct 27, 2021 23:08Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, shambulio la kimtandao dhidi ya vituo vya mafuta vya Jamhuri ya Kiislamu ni njama za maadui zilizolenga kuwahamakisha na kuvuruga maisha ya kila siku ya Wairani.
-
Njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Afghanistan ni kuzishirikisha kaumu zote katika muundo wa kisiasa
Oct 27, 2021 23:02Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Jrani na Afghanistan mwishoni mwa kikao chao hapa Tehran wametoa taarifa ya pamoja na kusisitiza kuwa: njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Afghanistan ni kuasisi muundo mpana wa kisiasa kwa kuyashirikisha makundi yote ya nchi hiyo.
-
Iran na EU zajadili namna ya kuondolewa vikwazo vyote haramu katika JCPOA
Oct 27, 2021 10:28Ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Ulaya imetangaza kuwa, kuondolewa vikwazo vyote haramu na visivyo vya kisheria ilivyoekewa Iran ndio ajenda kuu ya mazungumzo ya Brussels kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa na mratibu wa kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.