Khatibzadeh: Hakuna mawasiliano ya aina yoyote baina ya Iran na Marekani
-
Saeed Khatbizadeh
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amekadhibisha madai ya kuwepo mawasiliano baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekkani.
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya nchi za Maghariibi kwamba Marekani imeipendekezea Iran kufanya mazungumzo ya pande mbili, Saeed Khatbizadeh amesema leo mjini Tehran kwamba, hakujafanyika mazungumzo ya aina yoyote baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani kwa muda mrefu.
Khatbizadeh ameongeza kuwa, msimamo wa Iran kuhusu suala hilo uko wazi; Marekani imekiuka azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama na kujiondoa katika makubaliano ya nyukliia ya JCPOA na kisha ikafanya jitihada za kuharibu makubaliano hayo na baadaye ikaiwekea Iran vikwazo vya kidhalimu na knyume na sheria, hivyo hakuna mamawasiliano ya aina yoyote baina ya Iran na Marekani hadi pale hali hiyo itakapobadilika.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu na fatwa ya Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu, Iran haijawahi kuwa na nia ya kumiliki silaha za maangamizi ya umati na suala hilo halina nafasi yoyote katika ilani yake ya masuala ya ulinzi.
Amesema dunia nzima inapaswa kuchukua hatua za kuangamiza silaha za maangamizi ya umati na kuongeza kuwa, Marekani ndiyo nchi pekee duniani iliyotenda jinai dhidi ya binadamu kwa kutumia silaha za nyuklia.