-
Iran: Ni Marekani ndiyo yenye wajibu wa kurudi kwenye JCPOA
Jan 29, 2021 09:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, hivi sasa ni Marekani ndiyo yenye wajibu wa kurejea kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kutekeleza ahadi na majukumu yake.
-
Iran na Kenya zasisitiza kupanuliwa ushirikiano kati ya mashirika ya teknolojia ya nchi mbili
Jan 29, 2021 09:41Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia, Dakta Sorena Sattari amesisitiza kupanuliwa ushirikiano wa kiteknolojia kati ya mashirika ya Iran na Kenya.
-
Qatar yaishukuru Iran; sisitizo la nafasi chanya ya Iran katika kuleta uthabiti na amani katika eneo
Jan 29, 2021 06:03Huku akisisitiza kuwa uhusiano wa Qatar na nchi mbili za Iran na Uturuki ni mzuri sana, Lolwah al Khater, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amezishukuru nchi hizo kwa kuwa pembeni ya taifa hilo wakati ilipokuwa chini ya mgogoro mkubwa wa kuzingirwa na majirani zake.
-
Iran yasema huenda ikapunguza kiwango cha ushirikiano wake na IAEA
Jan 28, 2021 23:22Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao Vienna amesema yumkini Tehran itatazama upya kiwango cha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA.
-
Kujitakia makuu serikali ya Biden kuhusu Iran na mapatano ya JCPOA
Jan 28, 2021 07:23Maafisa wa serikali mpya ya Joe Biden nchini Marekani ambao huko nyuma walikuwa wakitoa matamshi kinyume na msimamo wa serikali ya wakati huo ya nchi hiyo, hivi sasa wanaonyesha kuwa na mitazamo sawa, bali hata kutumia lugha ile ile ya serikali ya Donald Trump kuhusu Iran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yazindua 'Jumba la Ubunifu na Teknolojia' Nairobi, Kenya
Jan 28, 2021 00:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuzinduliwa Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Iran (IHIT) katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Kenya na hata nchi nyingine za kanda ya Afrika Mashariki.
-
Vaezi: Israel haina nguvu za kijeshi za kutoa pigo kwa Iran
Jan 28, 2021 00:47Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel hauna mpango, uwezo, nguvu wala mkakati wa kulishambulia kijeshi taifa hili.
-
Zarif: Iran iko tayari kushirikiana na Russia kuhusu maeneo ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi
Jan 27, 2021 00:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano wa Iran na Russia ni kwa ajili ya amani na uthabiti katika eneo. Ameongeza kuwa: "Tuko tayari kushirkiana na Russia katika masuala ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi."
-
Amir Abdolahian: Uhusiano wa Iran, China na Russia ni wa kiistratijia
Jan 26, 2021 07:40Mshauri Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uhusiano wa Tehran, Beijing na Moscow ni wa kiistratijia na kuongeza kuwa, uhusiano na nchi za dunia ambazo zilikuwa pamoja na wananchi wa Iran wakati wa hali ngumu umejengeka juu ya msingi na stratijia ya urafiki, ushirikiano na kuheshimiana.
-
Balozi wa Iran UN: Rais wa Marekani achukue hatua ya kwanza
Jan 26, 2021 04:05Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu haina mpango wowote wa kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Marekani Joe Biden, lakini inasubiri serikali mpya ya Washington ichukue hatua ya kwanza ya kuliondolea taifa hili vikwazo na kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.