Jan 26, 2021 11:10 UTC
  • Amir Abdolahian: Uhusiano wa Iran, China na Russia ni wa kiistratijia

Mshauri Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uhusiano wa Tehran, Beijing na Moscow ni wa kiistratijia na kuongeza kuwa, uhusiano na nchi za dunia ambazo zilikuwa pamoja na wananchi wa Iran wakati wa hali ngumu umejengeka juu ya msingi na stratijia ya urafiki, ushirikiano na kuheshimiana.

Mwandishi wa IRIB amemnukuu Hossein Abdollahian akiashiria kwamba Bunge la 11 la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi hivi sasa limeshafanya vikao zaidi ya 170 na wajumbe wa daraja mbalimbali wa nchi za kigeni kutoka mashariki hadi magharibi mwa dunia na kuongeza kuwa, msimamo wa Bunge la Iran katika uhusiano wake wa kigeni na katika upande wa diplomasia ya kibunge ni kuwa na uhusiano mzuri na nchi za dunia katika kulinda manufaa ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mshauri huyo Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa pia amesema, Tehran ina misimamo huru na inaendelea na misimamo na siasa zake za "Si Mashariki, Si Magharibi, bali ni Jamhuri ya Kiislamu."

Hossein Abdollahian Mshauri huyo Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran)

 

Amesema, tutaendelea kudhamini maslahi ya taifa kwa kushirikiana kiuadilifu na nchi nyingine za Mashariki na Magharibi na kutoa kigezo kizuri cha udiplomasia wa kibunge na siasa za kigeni.

Vile vile amesema, msimamo na siasa kuu za Iran ni kuishi kwa amani na usalama pia na nchi zote duniani hususa nchi za Asia na hasa hasa majirani zake. Msimamo wa Tehran ni wa kutatua masuala yanayojitokeza kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano wa nchi zote za eneo hili.

Tags