-
Balozi wa Syria Tehran: Uchokozi wa Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran ni ugaidi
Jul 25, 2020 22:11Balozi wa Syria mjini Tehran amesema, uchokozi wa ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria ni nembo na dhihirisho la ugaidi wa Marekani dhidi ya raia wakiwemo wanawake na watoto.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran yakemea vikali hatua ya ndege zakivita za Marekani ya kuhatarisha usalama wa ndege ya abiria ya Iran
Jul 24, 2020 09:19Msemaji wa Wizara Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekemea vikali hatua ya ndege mbili za kijeshi za Marekani ya kutishia usalama wa ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria na kusema: Habari zaidi kuhusu tukio hilo zinafanyiwa uchunguzi na hatua za dharura za kisiasa na kisheria zitachukuliwa baada ya kukamilika uchunguzi huo.
-
Ufunguo wa kutatua mgogoro wa Syria ni kulindwa mamlaka ya kujitawala na wananchi kuwa na nafasi katika utawala
Jul 24, 2020 08:54Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kulindwa mamlaka ya kujitawala, mipaka na uhuru wa kisiasa Syria ni mambo ya dharura na pia wanajeshi wote wa kigeni walioko Syria wanapaswa kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo mara moja.
-
Mousavi: Moto wa karibuni nchini Iran hauhusiani na hujuma za kimtandao
Jul 23, 2020 02:54Akijibu madai kuhjusu uharibifu na hujuma za kimtandao dhidi ya Iran, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, moto uliotokea hivi karibuni hapa nchini hausiani kivyovyote na hujuma za kimtandao.
-
Rouhani: Uhuru wa kujitawala na usalama wa Iran na Iraq vinafungamana
Jul 21, 2020 22:00Rais Hassan Rouhani wa Iran na Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi wamesema uhusiano wa Tehran an Baghdad unavuka mipaka ya nchi mbili hizi jirani, na kusisitiza kuwa: Uhuru wa kujitawala na usalama wa Iran na Iraq vina mfungamano mkubwa.
-
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani: Siasa za Trump dhidi ya Iran zimeshindwa
Jul 20, 2020 21:50Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa, siasa za Rais Donald Trump wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo sababu ya kushindwa Washington katika medani zote.
-
Araqchi akanusha madai ya kuwepo ofisi ya Taliban nchini Iran
Jul 19, 2020 10:06Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amekabidhisha vikali madai ya kipropaganda kuwa kundi la wapiganaji wa Taliban la Afghanistan lina ofisi hapa nchini. Sayyid Abbas Araqchi aidha amekanusha vikali uvumi wa uwepo wa kundi la Taliban hapa nchini Iran, kwa jina la "Baraza la Mashhad."
-
Zarif: Iran na Iraq zinapaswa kuwa macho na tayari kukabiliana na ugaidi
Jul 19, 2020 06:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Iraq daima zinapaswa kuwa macho na tayari kwa ajili ya kukabiliana na njama za magenge ya kigaidi kama vile Daesh (ISIS) katika eneo hili la Asia Magharibi.
-
Ni bora Marekani ikiri imeshindwa na Iran badala ya kutoa vitisho vya kipuuzi
Jul 19, 2020 06:34Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametuma ujumbe kupitia Twitter akimhutubu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwa kusema: "Itakuwa bora iwapo Washington itakiri kushindwa na Iran yenye nguvu badala ya kutoa vitisho vya kipuuzi na visivyoweza kutekelezeka."
-
Wanasayansi wa Iran wapiga hatua kubwa katika utengenezaji wa chanjo ya Corona
Jul 17, 2020 09:40Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema timu kadhaa za wanasayansi nchini zimepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na kirusi cha corona.