-
Uchaguzi wa Rais Algeria uliokuwa umepangwa kufanyika Julai 4 waakhirishwa
Jun 02, 2019 22:58Baraza la kikatiba nchini Algeria limetangaza kuakhirisha uchaguzi wa rais ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 4 na kusema sababu ya uamuzi huo ni ukosefu wa wagombea. Uamuzi huo utapelekea kuongezeka muda wa mpito wa kisiasa jambo ambalo yamkini likaibua hasira zaidi za waandamanaji.
-
China yajibu vitisho vya Marekani vya kuitaka Hong Kong izizuie meli za mafuta za Iran
Jun 02, 2019 02:28Serikali ya China imetupilia mbali vitisho vya Marekani vya kuitaka kuziwekea vikwazo meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zisitie nanga na kutoa huduma zake katika bandari ya Hong Kong.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq: Kuna baadhi hawaoni mambo mema ya Iran
Jun 01, 2019 22:06Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq, Nouri al-Maliki amesema kuwa, baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu ni wakaidi kupindukia na wanajifanya hawaoni nafasi muhimu na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kadhia ya Palestina na kupigania kwake usalama wa mataifa ya eneo hili.
-
Ripoti mpya ya IAEA kuhusu Iran; sisitizo la kufungumana Tehran na makubaliano ya JCPOA
Jun 01, 2019 22:04Licha ya tuhuma zinazotolewa na Marekani kwamba Iran haijatekeleza majukumu wala kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na hata imeituhumu nchi hiyo kuwa inafanya juhudi za kuunda silaha za nyuklia, lakini ripoti ya karibuni ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) inaeleza kuwa, Tehran inaendelea kuheshimu na kutekeleza majukumu yake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
China yapuuzilia mbali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jun 01, 2019 03:21Serikali ya China imepuuzilia mbali vikwazo vya mafuta vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Tehran na imeanza kuagiza shehena ya mafuta yake kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Juhudi za Marekani za kuiwekea Iran vikwazo vya mafuta; ukweli au madai tu?!
May 31, 2019 23:52Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuiondoa nchi yake katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA, alitangaza kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo katika hatua mbili, yaani vya mwezi Agosti na Novemba mwaka jana wa 2018.
-
Katika Siku ya Quds, Wairani wasisitiza kuhusu kuunga mkono ukombozi wa Wapalestina
May 31, 2019 06:29Wananchi wa Iran walioshiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds wametoa taarifa ya mwisho na kusisitiza kuwa lengo la ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa ni ukombozi wa Quds Tukufu, kukombolewa taifa madhlumu na lisilo na ulinzi la Palestina kutoka katika makucha ya Wazayuni maghasibu na jitihada za kuondoa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ramani ya dunia.
-
Viongozi wa Iran wahimiza kuungwa mkono malengo matukufu ya taifa la Palestina
May 31, 2019 05:35Viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamehimiza mno suala la kuungwa mkono malengo matakatifu ya taifa la Palestina sambamba na Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo imeadhimishwa leo na mamilioni ya wapenda haki kote ulimwenguni.
-
Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yafanyika katika Iran ya Kiislamu
May 31, 2019 03:32Maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika kote katika Iran ya Kiislamu hii leo tarehe 31 Mei 2019 Miladia sawa na Ramadhani 25 mwaka 1440 Hijria ambapo wananchi wa matabaka mbalimbali wameonyesha hasira zao dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina.
-
Madai ya uwongo na yasiyo na msingi wa Mfalme wa Saudi Arabia dhidi ya Iran
May 31, 2019 03:21Mfalme wa Saudi Arabia ameibua madai ya uwongo na yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kukabiliana na kile alichokitaja kuwa vitisho vya Iran.