China yapuuzilia mbali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53846-china_yapuuzilia_mbali_vikwazo_vya_marekani_dhidi_ya_iran
Serikali ya China imepuuzilia mbali vikwazo vya mafuta vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Tehran na imeanza kuagiza shehena ya mafuta yake kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2019 03:21 UTC
  • China yapuuzilia mbali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Serikali ya China imepuuzilia mbali vikwazo vya mafuta vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Tehran na imeanza kuagiza shehena ya mafuta yake kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mara ya kwanza meli kubwa ya kubeba mafuta ya China (PACIFIC BRAVO) imebeba shehena ya mafuta kutoka Iran kwenda China, tangu serikali ya Marekani ilipofuta kibali cha kuendelea kununua mafuta ya nchi hii. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haijatoa radiamali yoyote kufuatia meli hiyo ya China kubeba mafuta ya Iran ingawa ilitangaza kwamba meli yoyote itakayokiuka vikwazo hivyo vya upande mmoja vya Washington, itakabiliwa na hatua kali. Hivi karibuni meli ya PACIFIC BRAVO ilinunuliwa na benki moja inayomilikiwa na shirika la mafuta la China kwa ajili ya kurahisisha biashara ya mafuta kati ya Tehran na Beijing.

Meli ya kubeba mafuta ya PACIFIC BRAVO

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli ya PACIFIC BRAVO sio meli ya kwanza kubeba mafuta kutoka Iran kwenda China, hii ni kwa kuwa tarehe 16 Mei mwaka huu pia meli nyingine ya China yenye jina la MARSHAL ilibeba karibu tani laki moja na elfu 30 za mafuta ya Iran na kupakua shehena hiyo katika mji wa Zhoushan na hivyo ikawa imekiuka vikwazo vya Marekani. Tarehe 22 Aprili mwaka huu, serikali ya Marekani ilitangaza kuzifutia kibali cha kuendelea kununua mafuta ya Iran nchi kadhaa za dunia, hatua ambayo ilikabiliwa na upinzani mkali kieneo na kimataifa.