-
Araqchi: Afisa wa IAEA Tehran, lakini hakuna mpango wa kukaguliwa maeneo ya nyuklia
Aug 11, 2025 05:37Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) anatarajiwa kufanya ziara hapa Tehran kwa mazungumzo, lakini kutembelea taasisi za nyuklia si sehemu ya ajenda ya safari hiyo.
-
Iran yazindua kliniki 9 kote nchini za kutibu majeraha kwa kutumia plasma
Aug 11, 2025 05:35Mohammad Eslami, Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) ametangaza kuzinduliwa kliniki tisa maalumu kote nchini zinazotumia plasma kutibu majeraha.
-
Velayati: Ikiwa na Russia au bila ya Russia, Iran itaukwamisha ushoroba wa Marekani eneo la Qafqaz
Aug 09, 2025 23:48Ali Akbar Velayati, Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itapinga kuanzishwa ushoroba wa usafirishaji na wa nishati unaodhibitiwa na Marekani nchini Armenia, jambo ambalo amesema litasababisha hatari kubwa kwa utulivu wa kanda hii.
-
Ayatullah Khamenei amteua Larijani kuwa mwakilishi wake katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa
Aug 07, 2025 22:48Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amemteua mwanasiasa mkongwe, Ali Larijani, kuwa mwakilishi wake katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC)
-
Iran yamnyonga gaidi wa kitakfiri wa Daesh aliyepatikana na hatia
Aug 06, 2025 09:03Mamlaka za Mahakama nchini Iran zimemnyonga mwanachama wa kundi la kigaidi na Kitakfiri la Daesh aliyepatikana na hatia ya kufanya mashambulizi ya kigaidi hapa nchini.
-
Ali Larijani ateuliwa Mkuu Mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran
Aug 06, 2025 04:30Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemteua mwanasiasa mkongwe Ali Larijani kuwa Mkuu Mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC).
-
Baqaei: Iran haiwezi kuiamini Marekani baada ya kushambulia vituo vyake vya nyuklia
Aug 05, 2025 11:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa nchi hii haiiamini Marekani khasa baada ya mashambulizi yake yasiyo na msingi katika vituo vya nyuklia vya Iran vinavyoendesha shughuli zake kwa malengo ya amani.
-
Iran yaalani hatua mpya za Wazayuni wenye misimamo ya mikali za kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa
Aug 04, 2025 04:09Esmaeil Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali kitendo cha Wazayuni wenye misimamo mikali cha kuuvunjia heshima kwa mara nyingine tena Msikiti wa Al-Aqsa wakiongozwa na waziri mtenda jinai wa utawala huo ghasibu Itamar Ben-Gvir ambaye ni Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel.
-
Nchi za Magharibi zinaonyesha sura hasi kuhusu Iran ili kushughulisha maoni ya umma kutokana na mizozo ya ndani
Aug 02, 2025 10:34Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar iliripoti mnamo Julai 31, 2025 kwamba Uingereza na nchi zingine 13 ziliituhumu Iran kuwa inapanga kufanya mauaji na utekaji nyara katika nchi za Magharibi, madai ambayo yamekanushwa vikali na Tehran.
-
Iran yakadhibisha madai hewa ya US na nchi zingine chache za Magharibi dhidi yake
Aug 01, 2025 04:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hatua ya Marekani, Ufaransa na nchi nyingine kadhaa za Magharibi ya kukariri tuhuma zisizo na msingi na za kuchekesha dhidi ya Iran na kuzielezea kuwa ni jaribio la waziwazi la kutaka kubebesha lawama wasiohusika na hila ya kuzibabaisha fikra za umma duniani ziachane na suala muhimu zaidi la wakati huu, yaani mauaji ya kimbari katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.