-
Pezeshkian: Hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuimarisha amani na usalama katika eneo
Dec 30, 2024 09:11Rais Masoud Pezeshkian ameeleza kuwa mtazamo na hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za kueneza amani na kudumisha usalama katika ukanda huu na baina ya nchi zote za Kiislamu; na ametaka kuwepo ushirikiano mkubwa zaidi kati ya Iran na Oman katika uwanja huo.
-
Araghchi asisitiza kuundwa serikali jumuishi nchini Syria
Dec 30, 2024 09:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia wajibu wa kuundwa serikali jumuishi nchini Syria. Sayyid Abbas Araqchi ameeleza haya leo katika kikao na waandishi wa habari hapa Tehran akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaidi.
-
Mcheza chess wa Iran akataa kushindana na mpinzani wa Israel akiwaunga mkono Wapalestina
Dec 30, 2024 00:15Katika kuwaunga mkono watu wa Palestina, mchezaji wa chess wa Iran amekataa kushindana na mwakilishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashindano ya World Rapid Chess Championship 2024 huko New York.
-
Ulyanov: Nchi za Magharibi zinazuia mazungumzo kati ya Iran na IAEA
Dec 28, 2024 04:00Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika mashirika ya kimataifa yenye makao yake makuu mjini Vienna amesema mbinu haribifu za nchi za Magharibi ni kikwazo cha maendeleo katika mazungumzo kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ili kusuluhisha masuala ambayo bado hayajatatuliwa.
-
Araqchi: Kuvuka kipindi cha sasa kunahitaji kujiepusha na mifarakano
Dec 28, 2024 03:59Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amewaambia maafisa wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: Kuvuka kipindi hiki chenye taharuki nyingi katika eneo la Magharibi mwa Asia kunahitaji busara, ushirikishwaji, ushirikiano na kuepusha mizozo na kujitakia maslahi ya muda mfupi.
-
Iran na Saudi Arabia kuimarisha uhusiano katika sekta ya teknolojia
Dec 27, 2024 23:14Rais wa Shirika la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano la Iran na Rais wa Kamati ya Mawasiliano, Anga za Mbali na Teknolojia (CST) ya Saudi Arabia katika mkutano wa pamoja huko Riyadh wamesisitiza kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
-
Russia yajibu matamshi ya Grossi kuhusu Iran: IAEA inapaswa kutoegemea upande wowote
Dec 26, 2024 06:54Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, amejibu matamshi ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), akisisitiza kwamba wakala huo haupaswi kusalimu amri kwa fikira potovu za nchi za Magharibi kuhusiana na suala la Iran.
-
Barua ya Iran kwa Baraza la Usalama baada ya Israel kukiri ilihusika na mauaji ya Ismail Haniyeh
Dec 25, 2024 08:37Amir Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa jana Jumanne alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisisitiza kwamba, Israel imebeba dhima ya kuhusika na mauaji ya Shahidi Ismail Haniyeh, mkuu zamani wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas.
-
Iran: Tuko tayari kufungua tena ubalozi Syria, tunafanya mazungumzo na serikali ya Damascus
Dec 24, 2024 09:22Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza utayarifu wa Tehran kufungua tena ubalozi wake mjini Damascus, huku kukiwa na changamoto zinazoikabili Syria wiki mbili baada ya wanamgambo wa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) kushika hatamu za nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran: Hatuna mawasiliano ya moja kwa moja na mrengo tawala wa sasa huko Syria
Dec 23, 2024 23:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa tulikuwa na mawasiliano na mrengo wa upinzani wa Syria tangu kitambo nyuma na tulisema kwamba Iran iliingia Syria kwa ajili ya kupambana na genge la kigaidi la Daesh (ISIS) na kuzuia kuenea ugaidi katika nchi za eneo hili, lakini hatuna mawasiliano ya wa moja kwa moja na mrengo uliotwaa madarakan nchini Syria hivi sasa.