-
Pentagon yakadhibisha madai ya Trump, yasema Daesh bado inaendesha shughuli zake Iraq na Syria
Aug 07, 2019 23:31Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 19 Disemba 2018 alitangaza kuwa, askari wa Marekani wataondoka nchini Syria. Trump alidai kuwa, sababu ya uamuzi huo ni kushindwa kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria.
-
Mwanamichezo wa Iraq aliyekataa kupambana na Mzayuni katika mashindano ya Thailand alakiwa kishujaa
Aug 07, 2019 23:31Ali al-Kanani, mwanamichezo wa Kiiraqi wa mchezo wa Ndondi za Kiki (Kickboxing), ambaye alikataa kupambana na mwanamichezo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashindano ya kimataifa ya mchezo huo yaliyofanyika nchini Thailand, amelakiwa kishujaa na wananchi wa Iraq alipowasili uwanja wa ndege wa kimatiafa wa Baghdad.
-
Iraq yatahadharisha kuhusu hatari ya mashambulizi ya wanawake Madaesh katika nchi mbalimbali
Aug 04, 2019 20:54Mkurugenzi wa Kitengo cha Kupambana na Ugaidi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ametahadharisha kuhusu hatari ya wanawake wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh wanaoelekea katika baadhi ya nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi.
-
Trump atishia kuwaachilia magaidi wa Daesh warejee katika nchi za Ulaya
Aug 02, 2019 07:27Marekani imekuwa na nafasi muhimu katika kubuni na kueneza shughuli za makundi ya kigaidi likiweo la Daesh katika mgogoro wa Syria kwa lengo la kuindoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo.
-
Vyombo vya ujasusi vya Iraq: Kiongozi wa Daesh yuko Syria, amepooza viungo vya mwili
Jul 29, 2019 22:29Kundi la Vipanga (Falcons) la shirika la upelelezi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq limetangaza kuwa, kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh, Abu Bakr al Baghdadi amejificha Syria na angali na satua baina ya wafuasi wa kundi hilo japokuwa amepooza viungo.
-
Mkuu wa Muungano wa al Fat'h asema, watawala wa Bahrain watakumbwa na hatima kama ya Saddam na Gaddafi
Jul 28, 2019 11:21Mwenyekiti wa Muungano wa al Fat'h nchini Iraq amesema kuwa hatua ya utawala wa Bahrain ya kuwanyonga vijana wawili wa nchi hiyo kwa tuhuma bandia ina maana ya mwisho wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa sawa kabisa na hatima iliyowapata madikteta walioangamizwa wa Iraq na Libya.
-
Waziri Mkuu wa Iraq atoa amri ya kuundwa tume ya uchunguzi ya kubaini ukweli
Jul 20, 2019 03:40Waziri Mkuu wa Iraq Adil Abdul-Mahdi ametoa amri ya kuundwa kamati ya uchunguzi kwa ajili ya kuchunguza shambulio la anga lililotekelezwa katika kambi ya Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi katika jimbo la Salah ad Din.
-
Waziri wa Mafuta wa Daesh (ISIL) auawa na askari wa Iraq nchini Syria
Jul 20, 2019 03:32Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Daesh ameangamizwa na vikosi vya kiintelijensia vya Iran katika mkoa wa Deir Ezzur, mashariki mwa Syria.
-
Marekani yaiwekea vikwazo harakati ya Hashd al Shaabi ya Iraq
Jul 19, 2019 01:54Naibu Rais wa Marekani amesema kuwa nchi hiyo imeamua kuwawekea vikwazo makamanda wanne waandamizi wa harakati ya wananchi ya Hashd al Shaabi ya Iraq.
-
Wabunge wa Iraq: Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ni kituo cha Mossad na Daesh
Jul 15, 2019 07:21Mbunge mwenye ushawishi mkubwa wa Iraq amefichua kwamba, ubalozi wa Marekani mjini Baghdad unajihusisha na harakati zinazotia wasiwasi na kwamba maajenti wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, na kundi la kigaidi la Daesh wamekuwa wakionekana wakiingia na kutoka katika jengo la ubalozi huo.