-
Buriani dola la "khilafa" bandia la Daesh
Jun 30, 2017 04:21Televisheni ya taifa ya Iraq jana ilitangaza rasmi habari ya kukomeshwa na kuangamizwa kundi la Daesh katika mji wa Mosul nchini humo. Habari hiyo iliyokosha na kufurahisha nyoyo za Wairaq na watu wengi wapenda haki na uadilifu kote duniani ilikuwa hitimisho la dola bandia la khilafa ya mawahabi la Daesh ambalo lilianzishwa Juni 2014 kwa ushirikiano wa chama cha Baathi kilichovunjwa huko Iraq, kwa msaada wa Saudi Arabia na washirika wake.
-
Waislamu wa Kisuni wa Mosul, Iraq wawakaribisha kwa shangwe wapiganaji wa Kishia
Jun 28, 2017 13:40Furaha na shamrashamra zimeshamiri na kuwatawala wakazi wa mji wa Mosul ambao ni wa Waislamu wa Kisuni katika kuwakaribisha wapiganaji wa Kishia wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi, kufuatia ushindi mkubwa uliofikiwa hadi sasa dhidi ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) mjini humo.
-
Waislamu duniani waungana kuswali na kusherehekea Iddil-Fitri
Jun 25, 2017 23:50Leo Waislamu wa maeneo tofauti duniani wanaungana katika swala ya Iddil-Fitri, baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa siku 30. Hapa Iran swala ya Iddil-Fitri imeswalishwa kitaifa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, hapa mjini Tehran muda mfupi uliopita.
-
UNESCO yaalani vikali hatua ya Daesh ya kubomoa msikiti wa kihistoria wa al Nuri
Jun 23, 2017 00:04Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limelaani vikali hatua ya kundi la kigaidi la Daesh ya kubomoa Msikiti wa kihistoria wa al Nuri katika mji wa Mosul nchini Iraq.
-
Rouhani: Ugaidi eneo la Mashariki ya Kati ni sehemu ya ajenda ya Israel
Jun 21, 2017 03:14Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema operesheni na harakati za kigaidi zinazoshuhudiwa katika eneo hili la Mashariki ya Kati ni sehemu ya ajenda ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa lengo la kuwashughulisha watu ili wasahau kadhia muhimu ya Palestina.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inapinga kura ya maoni ya kujitenga eneo moja la Iraq
Jun 20, 2017 12:42Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amepongeza umoja na mshikamano wa makundi yote ya kisiasa na kimadhehebu Iraq katika mapambano dhidi ya ISIS au Daesh na kusema uwepo wa 'Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi' ni tuko muhimu na lenye baraka ambalo ni chanzo cha nguvu nchini Iraq.
-
Kurejea Blackwater kwa jina jingine nchini Iraq; uwekezaji hatari mno wa Marekani
Jun 16, 2017 23:05Hivi sasa kumeenea habari za uwezekano wa kurejea nchini Iraq shirika la kihalifu la Blackwater la Marekani kwa jina jingine, suala ambalo limewakasirisha wananchi wa matabaka mbalimbali ya Iraq.
-
Syria: Sababu ya kutokea mashambulio ya kigaidi mjini Tehran hii hapa
Jun 14, 2017 11:06Balozi wa Syria nchini Iraq amesema kuwa, sababu kuu ya kutokea mashambulizi ya kigaidi mjini Tehran, ni kutokana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa nchi pekee iliyosimama kikweli na wananchi na serikali za Iraq na Syria kupambana na magenge ya kigaidi yaliyozivamia nchini hizo.
-
Watu 39 wauawa katika mashambulio ya mabomu ya magaidi wa Daesh Iraq
Jun 09, 2017 10:52Kwa akali watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyofanywa hii leo na kundi la kigaidi la Daesh katika miji ya Babil na Karbala nchini Iraq.
-
UN: wapiganaji wa Daesh wanawauwa watoto wanaokimbia vita Mosul
Jun 08, 2017 22:55Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh wanawapiga risasi watoto wanaokimbia vita na mapigano katika mji wa Mosul huko kaskazini mwa Iraq.