-
Iran: Reuters inaeneza habari 50 za uongo kila siku dhidi yetu; uanagenzi wa Trump ni kwa manufaa ya Tehran
Jun 24, 2018 10:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria hatua zisizo za kimantiki za rais wa Marekani ikiwa ni pamoja na uamuzi wake wa kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, matokeo ya hatua hizo ni kuzidi kuharibika jina la Donald Trump na kuzidi kunufaika Iran.
-
Araqchi: JCPOA ipo katika ICU, yumkini Iran ikajiondoa wiki chache zijazo
Jun 23, 2018 02:51Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita za kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yako chumba cha wagonjwa mahututi ICU, na yumkini Tehran ikajiondoa kwenye mapatano hayo ndani ya wiki chache zijazo.
-
UN: Kulindwa JCPOA kuna umuhimu kwa usalama wa dunia
Jun 20, 2018 02:59Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kulindwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni jambo lenye udharura mkubwa hususan katika kudhamini usalama wa dunia.
-
Boroujerdi: Matamshi ya nchi za Ulaya kuhusu JCPOA si utatuzi wa matatizo ya Iran
Jun 17, 2018 22:02Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, matamshi chanya ya viongozi wa nchi za Ulaya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA hayawezi kutatua matatizo ya Iran bali viongozi hao wanapaswa kuakisi misimamo yao kivitendo na watekeleze ahadi zao kwa kutokubaliana na misimamo ya Marekani.
-
Zarif arejea Tehran kutokea Afrika Kusini
Jun 14, 2018 10:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amerejea hapa Tehran leo asubuhi baada ya kumaliza ziara rasmi nchini Afrika Kusini ambako alionana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mbalimbali wa nchi hiyo.
-
Rouhani: Iran itajiondoa JCPOA iwapo haitadhaminiwa maslahi yake
Jun 13, 2018 02:45Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itajiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA iwapo itahisi haistafidi wala kupata maslahi yoyote kutokana na mapatano hayo ya kimataifa.
-
Larijani: Iran itachukua hatua muafaka kukabiliana na chokochoko za Marekani
Jun 12, 2018 09:38Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, Ali Larijani ameashiria hatua ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA, na kusema: 'Hatua hii ya Marekani imeathiri kwa kiasi fulani uwekezaji nchini, na ili kukabiliana na hilo, tayari hatua maufaka zimechukuliwa na mazungumzo yanaendelea."
-
Tahadhari kali ya Putin kuhusu athari mbaya za kujiondoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA
Jun 11, 2018 02:27Rais Vladimir Putin wa Russia amekosoa vikali uamuzi wa Marekani wa kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA akisema unatishia usalama na amani ya Mashariki ya Kati.
-
Kujitoa Marekani kwenye JCPOA na kupoteza itibari katika mazungumzo na Korea Kaskazini
Jun 09, 2018 02:40Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema, kuna ulazima wa kuyadumisha makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA na kubainisha kwamba: Wakati makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanalegalega, mwafaka wenye uwezekano wa kufikiwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini nao pia hautokuwa na itibari yoyote.
-
Zarif: Nchi wanachama wa JCPOA zifidie hasara ilizopata Iran bila kutoa masharti yoyote
Jun 08, 2018 00:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Ili makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yaendelee, lazima nchi zilizosalia kwenye makubaliano hayo pamoja na washirika wengine wa kibiashara watoe hakikisho kwamba hasara ilizopata Iran (kutokana na Marekani kujitoa kwenye JCPOA) zinafidiwa bila masharti yoyote kupitia hatua za kitaifa, kieneo na kimataifa.