Oct 09, 2023 08:13
Makundi ya muqawama ya Palestina yenye makao katika Ukanda wa Ghaza yaani harakati ya Hamas na harakati nyingine za Palestina khususan Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina juzi Jumamosi tarehe 7 Oktoba yalianzisha oparesheni kwa jina la Kimbunga cha Al Aqsa dhidi ya utawala wa Kizayuni; oparesheni iliyouduwaza kikamilifu utawala huo na kuwashtua pakubwa Wazayuni.