May 01, 2016 14:12 UTC
  • Iran yataka Wapalestina waungane kukabiliana na Utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo umoja miongoni mwa makundi yote ya Palestina.

Zarif ameyasema hayo leo mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Ramadhan Abdullah Shalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina. Katika kikao hicho, wawili hao walitathmini matukio ya hivi karibuni huko Palestina na eneo la Mashariki ya Kati kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Irana amesema leo umoja wa makundi yote ya Kipalestina ni jambo la dharura. Aidha amesisitiza kuwa, lengo la ulimwengu wa Kiislamu na makundi ya kupignia ukombozi wa Palestina ni kuondoa hatari ya utawala wa Kizayuni.

Zarifa amesema kadhia ya Palestiina ni kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, ni jambo lilislokubalika kudunisha hatari ya utawala wa Kizayuni.

Katibu Mkuu wa Jihad Islami kwa upande wake amewasilisha ripoti kuhusu hali ya mambo Palestina na eneo pamoja na nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika utatuzi wa matatizo ya eneo.

Tags