-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 15:56Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Mwili wa shahidi Qassem Soleimani na ya mashahidi wenzake yasindikizwa na kuagwa Ahvaz na Mashhad + Video
Jan 05, 2020 15:40Mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na ya mashahidi wenzake waliouliwa shahidi pamoja naye katika jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani imesindikizwa na kuagwa leo katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mwa Iran na huko Ahvaz kusini mwa nchi.
-
Marekani itabeba dhima ya chochote kitakachotokea baada ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 07:40Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Mohandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Al Hashd al Shaabi) pamoja na watu wengine 8 waliuawa shahidi mapema Ijumaa 3 Januari 2019 katika hujuma ya angani ya jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.
-
Pakistan yatoa radiamali kali kufuatia hujuma ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema kuwa, kitendo cha kigaidi kilichofanywa na Marekani cha kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, kitasababisha ukosefu wa amani katika eneo.
-
Maelfu ya Waislamu nchini India waandamana kulaani kuuliwa shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Maelfu ya Waislamu nchini India wamelaani vikali kitendo cha Marekani cha kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC.
-
Taathira za kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis
Jan 05, 2020 04:28Usiku wa manane wa kuamkia juzi Ijumaa Januari 3 viongozi wa Marekani walitekeleza kitendo cha kijinai na kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (Hashdu al Shaabi).
-
Salami: Marekani itajuta kumuua kigaidi Luteni Jenerali Soleimani
Jan 05, 2020 04:52Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa mpangaji wa mikakati iliyopoelekea Marekani ipate hasara za kistratijia na kuongeza kuwa: "Kuuawa kigaidi Jenerali Suleimani ni mwanzo wa kumalizika uwepo wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi."
-
Sheikh Zakzaky: Kuuawa shahidi Qassim Soleimani kutaimarisha zaidi ari ya mapambano
Jan 04, 2020 13:20Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na Naibu Mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al-Hashdul al-Shaabi, Abu Mahdi al-Muhandes kutapelekea kuimarika zaidi ari na moyo wa mapambano.
-
Umati mkubwa wausindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani mjini Baghdad
Jan 04, 2020 12:42Umati mkubwa wa watu umejitokeza leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliyeuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
-
Wapalestina: Sehemu kubwa ya juhudi za Shahidi Soleimani zilihusu ukombozi wa Palestina
Jan 04, 2020 07:45Brigedi za shahidi Izzuddin-al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekeza sehemu kubwa ya juhudi zake kwa ajili ya kuutokomeza na kuuangamiza utawala wa Kizayuni na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.