-
Uchunguzi wa maiti katika mauaji tata ya Shakahola, Kenya waondoa uwezekano wa kuwepo uvunaji wa viungo
May 08, 2023 10:23Uchunguzi wa kidaktari uliofanyiwa miili 112 ya wahanga wa mauaji tata ya Shakahola iliyofukuliwa katika makaburi mbalimbali katika kaunti ya Kilifi katika eneo la Pwani Kenya umeondoa uwezekano juu ya uwepo wa uvunaji viungo katika miili ya wahanga hao.
-
Rais wa Kenya: Nitatumia mamlaka yangu kama Amiri Jeshi Mkuu kuzuia maandamano ya Azimio
May 01, 2023 01:49Rais William Ruto wa Kenya amesema, yuko tayari kutumia mamlaka aliyonayo kama Amiri Jeshi Mkuu kuzuia maandamano ya Muungano wa Azimio la Umoja yaliyopangwa kufanyika kesho Jumanne yakiongozwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
-
Maiti za waliofariki katika kanisa lenye misimamo mikali Kenya zakaribia 100
Apr 27, 2023 10:48Idadi ya waathirika wanaoaminika kufa na njaa kutokana na imani kali ya Kikristo nchini Kenya imeongezeka na kufikia 98 hadi kufikia leo mchana, huku familia zingine zikisubiri habari za wapendwa wao ambao ni wafuasi wa kanisa hilo na hadi sasa hawajulikani waliko.
-
Raila Odinga kuanza tena maandamano dhidi ya serikali ya Kenya
Apr 24, 2023 12:35Mrengo wa upinzani nchini Kenya umesema kuwa umepanga kuanza tena maandamano dhidi ya serikali kuanzia tarehe Pili mwezi ujao wa Mei; ikiwa zimepita karibu wiki tatu tangu usimamishe maandamano yake dhidi ya serikali ya Rais William Ruto ili kutoa fursa ya kushiriki kwenye mazungumzo na serikali.
-
Ugonjwa wa Typhoid kali wasababisha vifo vya watu 4 huko Kakamega, Kenya
Apr 16, 2023 11:24Ripoti kuhusu mmlipuko wa ugonjwa ambao hadi sasa umeua watu wanne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mukumu katika Kaunti ya Kakamega huko Kenya inaashiria kisa cha homa ya matumbo iliyosababishwa na maji yaliyochafuliwa na baktera aina ya Salmonella Typhi.
-
Wabunge wa Kenya: Wanajeshi watenda jinai wa Uingereza wahukumiwe nchini
Apr 13, 2023 03:29Wanajeshi wa Jeshi la Uingereza wanaotoa mafunzo nchini Kenya wanaofanya mauaji nchini humo huenda wakakabiliwa na mashtaka katika mahakama za Kenya iwapo mapendekezo yaliyopendekezwa bungeni na Kamati ya Ulinzi na Mahusiano ya Kigeni yatapitishwa.
-
Wakenya wamtaka Rais Ruto, Raila wafanye muafaka wa kisiasa
Apr 10, 2023 05:47Rais William Ruto wa Kenya na kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, wako kwenye shinikizo la kubuni Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kurejesha utulivu wa kisiasa nchini Kenya.
-
Madaktari Kenya watahadharisha kuhusu aina mpya za magonjwa ya zinaa
Apr 03, 2023 09:52Madaktari wamewataka Wakenya kuwa na tahadhari baada ya kugunduliwa aina mbili mpya za magonjwa ya zinaa (STIs).
-
Mama: Askari wa Marekani waliomuua mwanangu ni wanyama
Mar 23, 2023 12:21Mama mzazi wa Ivor Otieno, kijana Mkenya aliyeuawa hivi karibuni na polisi ya Marekani akiwa korokoroni amewataja askari polisi waliofanya ukatili huo kuwa wanyama.
-
Kadhaa wajeruhiwa na kukamatwa katika maandamano ya wapinzani Kenya, Afrika Kusini
Mar 20, 2023 14:01Maafisa usalama nchini Kenya wametumia mabomu ya gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kukabiliana na wafuasi wa kinara wa upinzani nchini humo Raila Odinga, ambao wamejitokeza kwa wingi kushiriki maandamano ya nchi nzima dhidi ya serikali ya Rais William Ruto.