-
Serikali ya Libya yatangaza kafyu katika mji mkuu Tripoli
Aug 27, 2020 02:08Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imetangaza kuweka kafyu katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli kufuatia kushtadi maandamano ya wananchi.
-
Wanamgambo wa Haftar wakosoa pendekezo la Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya
Aug 24, 2020 22:59Msemaji wa wanamgambo wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftari ambao wanajiita Jeshi la Kitaifa la Libya wamepinga pendekezo lililotolewa na kiongozi wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya na kulitaja kama la kuleta mshawasha kwa fikra za waliowengi nchini humo.
-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya yatangaza kusitisha vita
Aug 22, 2020 19:31Wakati pande mbalimbali zikiendelea kulumbana juu ya namna ya kugawana keki ya Libya na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo, Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli imetoa amri ya kusitishwa vita mara moja na kusimamishwa operesheni zote za kijeshi.
-
Guterres atoa wito wa kuanza mchakato wa kisiasa kwa ajili ya amani nchini Libya
Aug 22, 2020 04:41Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande mbili hasimu katika mgogoro wa Libya kujiunga na mchakato wa kisiasa wa kutafuta suluhisho la matatizo ya nchi hiyo.
-
Wahajiri 45 wafariki katika pwani ya Libya kwenye ajali mbaya zaidi ya meli mwaka huu
Aug 20, 2020 02:39Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameripoti kuwa, wahamiaji wasiopungua 45 kutoka nchi za Afrika pamoja na wakimbizi wamefariki dunia katika Bahari ya Mediterania kwenye ajali mbaya zaidi ya baharini kutokea katika pwani ya Libya katika mwaka huu wa 2020.
-
Uturuki, Qatar na Libya kushirikiana kijeshi
Aug 18, 2020 10:13Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imesema imefikiana na Uturuki na Qatar juu ya kutia saini mkataba wa pande tatu wa ushirikiano wa kijeshi na kwamba miongoni mwa nukta muhimu za ushirikiano huo ni kujenga kituo cha kijeshi cha Uturuki katika Bandari ya Misrata nchini Libya.
-
Uturuki na Libya zasaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi yenye thamani ya dola bilioni 16
Aug 16, 2020 21:58Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli imesaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na Uturuki yenye thamani ya dola bilioni 16.
-
Wananchi wenye hasira wachoma moto ubalozi wa Imarati nchini Libya
Aug 16, 2020 07:03Wananchi wa Libya wenye hasira wamechoma moto jengo la ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mjini Tripoli wakilalamikia hatua ya serikali ya Abu Dhabi ya kufikia makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel.
-
Wapiganaji wa Janjaveed wa Sudan wapelekwa Libya kujiunga na Haftar
Aug 11, 2020 06:53Jeshi la Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa nchini Libya limetangaza kuwa mfasara uliokuwa na magari 70 ya kijeshi yakibeba silaha na mamluki wa kundi la Janjaweed umevuka maeneo maarufu kama Hilali ya Mafuta ya Libya ukiuelekea katika mji wa Sirte kwa ajili ya kumsaidia jenerali muasi, Khalifa Haftar.
-
Mkuu wa Shirika la Mafuata Libya: Maafa makubwa zaidi ya yale ya mlipuko wa Beirut yanainyemelea Libya
Aug 09, 2020 23:55Mkuu wa Bodi ya Shirika la Taifa la Mafuta nchini Libya ametahadharisha kuwa maafa makubwa zaidi kuliko yale yaliyosababishwa na mlipuko uliotokea katika bandari ya Beiruti yanainyemelea Libya kutokana na kusitisha uuzaji nje mafuta ya nchi hiyo na kurundikwa bidhaa hiyo katika maghala.