-
ICC yatakiwa kuzipatia kipaumbele jinai zinazojiri mashariki mwa Kongo
Dec 07, 2022 15:03Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amemtaka Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya ICC kuchunguza mauaji ya halaiki yaliyojiri wiki jana katika mji wa Kishishe mashariki mwa Kongo.
-
Kabuga, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda akwepa ufunguzi wa kesi yake
Sep 29, 2022 12:21Felicien Kabuga anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda ameripotiwa kukataa kuhudhuria ufunguzi wa kesi dhidi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya mjini Hague nchini Uholanzi.
-
Iran yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya mahakama ya ICC
Dec 09, 2021 04:41Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Venezuela yaitaka ICC ichunguze vikwazo vya Marekani dhidi yake
Aug 25, 2021 12:56Makamu wa Rais wa Venezuela ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ifanye uchunguzi juu ya vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, akisisitiza kuwa vikwazo hivyo ni jinai dhidi ya binadamu.
-
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kufungua ofisi Sudan
Aug 13, 2021 23:59Sudan na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake huko Hague, Uholanzi zimesaini makubaliano ya ushirikiano kama hatua moja mbele katika jitihada za kushughulikia kesi ya dikteta wa zamani wa Sudan, Omar Hassan al Bashir ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.
-
Sudan yaazimia kujiunga na mahakama ya kimataifa ya ICC
Aug 05, 2021 02:32Serikali ya Sudan imechukua hatua ya kwanza ya kutaka kujiunga na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
ICC yabatilisha waranti wa kukamatwa mke wa aliyekuwa rais wa Kodivaa
Jul 30, 2021 12:41Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetupilia mbali waranti wa kukamatwa Simone Gbagbo, mke wa Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa Ivory Coast.
-
Bensouda aitaka Sudan iikabidhi ICC watuhumiwa wa jinai za Darfur
Jun 10, 2021 12:28Kwa mara nyingine tena, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amewataka maafisa wa serikali ya Sudan kuwakabidhi watuhumiwa wa jinai za kivita katika eneo la Darfur kwa mahakama hiyo, akiwemo rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar Hassan al Bashir.
-
ICC yamhukumu Ongwen kifungo cha miaka 25 jela
May 06, 2021 12:42Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wamemhukumu kifungo cha miaka 25 jela Dominic Ongwen, mwanajeshi mtoto wa zamani wa Uganda ambaye alikuwa kamanda wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army (LRA), baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu nchini Uganda.
-
Mshukiwa wa Sudan anayesakwa kwa jinai za Darfur afadhilisha ICC
May 05, 2021 06:18Afisa wa zamani wa serikali ya Sudan anayetuhumiwa kuhusika na jinai zilizofanyika katika eneo la Darfur amesema anafadhilisha kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC badala ya faili lake kusikilizwa nchini Sudan.