Jul 19, 2022 14:34
Ghasia machafuko ya kikabila yaliyoanzia katika Jimbo la Blue Nile nchini Sudan yamepanuka zaidi na kuingia katika majimbo kadhaa ya nchi hiyo, huku maelfu ya watu wa kabila la Hausa wakiandamana na kufunga barabara katika maeneo kadhaa kupinga ghasia hizo, ambazo wanasema ziliwalenga wao katika Jimbo la Blue Nile.