-
Anthony Cordesman: Shambulizi dhidi ya meli lilifanywa na ISIS, Saudia na Imarati
Jun 16, 2019 07:31Anthony Cordesman, mchambuzi wa kisiasa wa nchini Marekani kuhusu masuala ya Iran amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio la kushambuliwa meli mbili za mafuta za Japan katika bahari ya Oman, lilifanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), Saudia na Imarati.
-
Marais wa Iran na Uturuki wakosoa sera za vikwazo na mashinikizo
Jun 16, 2019 03:14Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zinapinga vikali sera za vikwazo, mashinikizo na uchukuaji maamuzi ya upande mmoja kwenye uhusiano wa kimataifa.
-
India yajibu mapigo, yatangaza ushuru wa juu kwa bidhaa za Marekani
Jun 16, 2019 02:22Serikali ya India imetangaza ushuru wa juu wa forodha kwa bidhaa 28 za Marekani, ikiwa ni radimali ya nchi hiyo ya Asia kwa vikwazo vya kibiashara vya Washington dhidi yake.
-
Moscow yailaumu Marekani kwa kuibua mivutano Asia magharibi
Jun 15, 2019 21:46Marekani katika kipindi hiki cha utawala wa Rais Donald Trump imeanzisha jitihada za kuasisi muungano na kuimarisha uwepo wake katika eneo la Asia magharibi hususan katika Ghuba ya Uajemi kwa kisingizio cha eti kuwepo vitisho kutoka kwa Iran.
-
Sanders na Corbyn: Shambulio la Bahari ya Oman lisitumike kuanzisha vita
Jun 15, 2019 06:24Viongozi mashuhuri wa kisiasa nchini Marekani na Uingereza wameionya vikali serikali ya Washington, dhidi ya kutumia tukio la kushambuliwa meli za mafuta katika Bahari ya Oman kama kisingizio cha kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Guterres ataka uchunguzi huru wa kushambuliwa meli za mafuta Bahari ya Oman
Jun 15, 2019 03:45Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru wa tukio la kushabuliwa meli za mafuta katika Bahari ya Oman.
-
Ukosoaji mkali wa Sweden na Russia kwa mienendo hasi ya Marekani kuhusu mapatano ya JCPOA
Jun 15, 2019 03:04Hatua ya Marekani ya kujiodoa kwenye mapatano ya nyukali ya JCPOA hapo mwezi Mei 2018 na kisha kurejesha vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran katika hatua mbili, sambamba na kukosolewa na wanachama wa kundi la 4+1, imekosolewa pia na nchi nyingine katika ngazi ya kimataifa kama vile Sweden.
-
Gazeti la Al-Quds Al-Arabi: Saudia na Israel zinachochea migogoro katika eneo
Jun 15, 2019 00:11Gazeti la Al-Quds Al-Arabi linalochapishwa London, Uingereza limeandika kuwa, baadhi ya pande katika eneo la Asia Magharibi hususan Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel, zinahusika kushadidisha migogoro katika eneo.
-
Ayatullah Khatami: Taifa la Iran halitafanya mazungumzo kutokana na mashinikizo
Jun 14, 2019 08:33Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa kufanya mazungumzo na Marekani hakuna faida yoyote, na taifa la Iran kamwe halitafanya mazungumzo chini ya mashinikizo ya kiuchumi.
-
Kiongozi Muadhamu: Trump hana ustahiki wa kupewa ujumbe, hatufanyi mazungumzo na Marekani
Jun 13, 2019 07:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiiamini Marekani hata kidogo na uzoefu mchungu wa mazungumzo yaliyotangulia na Marekani katika fremu ya JCPOA kamwe hayatarudiwa tena kwani hakuna taifa lolote lililo huru na lenye akili litakalokubali kufanya mazungumzo chini ya mashinikizo."