-
Iran: Marekani ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza
Oct 25, 2023 04:07Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Marekani ni mshirika katika jinai za kutisha za Israel huko Ukanda wa Gazal kutokana na uungaji mkono wake usio na kifani kwa utawala huo unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Uganda yataja onyo la Marekani dhidi yake kuwa kichekesho
Oct 25, 2023 04:06Uganda imekejeli na kukosoa tahadhari iliyotolewa na Marekani iliyodai kuwa ni hatari kufanya biashara na kuwekeza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Upinzani mkali wa Marekani dhidi ya juhudi za kusitisha vita Ghaza
Oct 24, 2023 06:33Marekani ikiwa ni mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni si tu kwamba inatoa misaada ya kila aina ya silaha na fedha kwa ajili ya kuushambuliwa Ukanda wa Ghaza, bali pia inapinga vikali usitishwaji vita katika uvamizi huo wa umwagaji damu kwa visingizio vya uongo na visivyo na msingi.
-
Gaza: Israel imevunja kabisa misikiti 31 na kuharibu vibaya makanisa 3
Oct 22, 2023 11:27Ofisi ya Vyombo ya Habari vya Serikali ya Ukanda wa Gaza imetangaza leo Jumapili kwamba idadi ya misikiti iliyovunjwa kabisa katika mashambulizi ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia misikiti 31, na uharibifu mkubwa umerekodiwa katika makanisa 3.
-
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia: Marekani itashindwa huko Ukraine kama ilivyofeli Afghanistan
Oct 21, 2023 23:50Balozi wa Korea Kaskazini nchini Russia amelaani uungaji mkono na misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine na kusema, mara hii pia Marekani itashindwa na kufeli kama ilivyokuwa huko Afghanistan.
-
Ukosoaji wa Russia kwa siasa za uadui za Marekani ulimwenguni
Oct 21, 2023 03:54Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Russia amekosoa vikali siasa za uhasama za Marekani ulimwenguni.
-
Kikao kisichokuwa na natija cha Baraza la Usalama: Marekani yapinga usitishaji mapigano Gaza
Oct 19, 2023 07:20Jumatano, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikataa tena azimio la kusitisha mapigano huko Gaza kufuatia upinzani wa Marekani. Marekani ilipinga azimio lililopendekezwa kwa Baraza la Usalama na Brazil, lililotaka kusitishwa mapigano ili kufikishwa misaada ya kibinadamu Ghaza.
-
Kiongozi Mkuu wa Iran: Jinai za Gaza zisiposimamishwa, hakuna atakayeweza kuwazuia Waislamu na Wanamuqawama
Oct 17, 2023 08:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: wananchi wa mataifa ya Kiislamu na hata watu wasio Waislamu duniani wamekasirishwa sana na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala unaoikalia Quds kwa mabavu, na iwapo unyama na ushenzi huo utaendelea Waislamu duniani na vikosi vya Muqawama wataishiwa na subira na hakuna atakayeweza kuwazuia.
-
Hamas: Nchi zinazounga mkono mashambulizi ya Israel zinahusika katika mauaji ya watoto na wanawake
Oct 17, 2023 00:17Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ilisema jana Jumatatu kuwa, nchi zinazounga mkono uvamizi wa Israel katika hujuma yake inayoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa zinahusika katika mauaji ya watoto, wanawake na raia.
-
Kukaririwa mauaji ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watoto huko Marekani kwa kuuawa kinyama mtoto wa Kipalestina
Oct 16, 2023 08:43Polisi ya Chicago imetangaza kuwa mkazi mmoja wa mji huo amemuua mvulana wa Kipalestina wa miaka 6 kwa kisu na kumjeruhi vibaya mama yake.