Jan 05, 2024 07:46 UTC
  • Hassan Sharif
    Hassan Sharif

Imamu wa Msikiti wa Muhammad huko Newark, katika jimbo la New Jersey nchini Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi mbele ya msikiti huo.

Tovuti ya USA Today imeripoti kuwa, Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la New Jersey, Matthew Plotkin amesema kuwa jina la mwathiriwa ni Hassan Sharif, na kwamba alifariki dunia kutokana na majeraha akiwa hospitalini baada ya kupigwa risasi kadhaa Jumatano asubuhi.

Plotkin ameongeza kuwa lengo la uhalifu huo bado halijajulikana lakini amedai kuwa ushahidi uliokusanywa hadi sasa hauonyeshi kwamba uhalifu huo umetokana na sababu za ubaguzi wa rangi au ugaidi.

Msikiti wa Muhammad huko Newark, katika jimbo la New Jersey

Mwanasheria Mkuu wa New Jersey amesema: "Kwa kuzingatia matukio ya kimataifa na chuki inayoongezeka ambayo inalenga jumuiya nyingi katika jimbo la New Jersey, hasa jamii ya Kiislamu, watu wengi sasa wanakabiliwa na hali ya hofu kubwa." 

Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) kwa kifupi tawi la New Jersey limetangaza kuwa linafanya kazi kupata taarifa zaidi kuhusu sababu za mauaji hayo.

Wakazi laki tatu (300,000) huko New Jersey ni Waislamu.

Tags