Vyama vya upinzani Israel vyaafikiana kuvunja Bunge
(last modified Thu, 12 Jun 2025 02:11:52 GMT )
Jun 12, 2025 02:11 UTC
  • Vyama vya upinzani Israel vyaafikiana kuvunja Bunge

Kanali ya 13 ya televisheni ya Kiebrania imeripoti kwamba vyama vya upinzani Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu) zimeafikiana kuidhinisha pendekezo la kisheria kuhusu kuvunjwa Bunge la utawala wa Kizayuni (Knesset).

Kwa mujibu wa taarifa, vyama vya upinzabni vya utawaola wa Kizayuni vimetoa taarifa yenye madhumuni yasemayo: Viongozi wa vyama vya upinzani wanakubaliana na Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu kupigiwa kura pendekezo la kisheria la kuvunjwa Bunge. Huu ni uamuzi wa pamoja ambao ulichukuliwa wakati wa kikao cha viongozi wa vyama vya upinzani.

Vyama vya Lena na Yisrael Beit nu vimetangaza kuunga mkono suala hilo Ivigdor Lieberman," kiongozi wa chama cha "Israel Beit nu", amesema mbele ya waandishi wa habari kwamba, serikali ya sasa inapaswa kuvunjwa tarehe 7 Oktoba mwaka huu. Hayo yanajiri sambamba na kuongezeka mashinikizo dhidi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel.

Mashinikizo ya vuguvugu la upinzani katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina (Israel) ya kutaka kumpindua Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na baraza lake la mawaziri yameongezeka. Netanyahu anakabiliwa na shutuma kali kutoka kwa familia za mateka wa Israel.

Familia hizo zinamnyooshea kidole cha lawama kwa kushindwa kufikia makubaliano ya kumaliza vita na kubadilishana mateka na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Wapinzani wa Netanyahu hasa familia za mateka ambao ndugu zao wanashikiliwa na HAMAS wanasema kuwa, kuendelea vita hakuna natija ghairi ya kuongeza masaibu na machungu kwa pande zote mbili.