-
Mkuu wa majeshi ya Marekani akiri rasmi kuwa wameshindwa katika vita vya Afghanistan
Sep 15, 2023 22:55Mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Mark Milley amekiri kuwa vita ilivyoanzisha nchi hiyo huko Afghanistan vimeishia kwa kushindwa vikosi vya jeshi hilo.
-
Hatua mpya ya Baraza la Wawakilishi la Marekani dhidi ya Iran; jaribio la kuzidisha mashinikizo
Sep 15, 2023 22:45Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha mpango wa kiuadui dhidi ya Iran unaojulikana kama "Sheria ya Mahsa" kwa kura 410 za ndio na 3 za hapana. Mpango huo unailazimu serikali ya Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wakuu wa Iran kwa kisingizio cha haki za binadamu, na wakati huo huo kupiga marufuku kuingizwa na kuuzwa nje silaha za Iran.
-
Njama mpya za Marekani za kushadidisha vita vya Ukraine
Sep 13, 2023 22:53Viongozi wa Marekani wametangaza kuwa, serikali ya Joe Biden imekaribia kupasisha muswada wa kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba mabomu ya vishada.
-
Kuendelea kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na siasa za kindumakuwili za Magharibi
Sep 10, 2023 22:57Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amezungumzia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nje ya ubalozi mdogo wa Uturuki mjini New York na kubainisha kwamba, kudharau vitabu vitakatifu ni jambo la kuchukiza.
-
Moscow: Marekani inatafakari kuwaua viongozi wa mapinduzi Niger
Sep 08, 2023 03:49Shirika la Kijasusi la Russia nje ya nchi (SVR) limeonya kuwa, serikali ya Marekani inatafakari suala la kuwaua kigaidi viongozi walioongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.
-
Hatua mpya ya Marekani ya kukoleza moto wa vita: Kuipelekea Ukraine risasi zenye madini ya urani
Sep 03, 2023 05:19Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani imeamua kwa mara ya kwanza kuipatia Ukraine risasi zenye madini ya urani hafifu. Risasi hizo ni sehemu ya shehena mpya ya silaha ambayo itatangazwa mnamo siku zijazo.
-
Iran yakosoa uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Kibinadamu la UN
Sep 02, 2023 08:00Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amekosoa uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo.
-
Ansarullah yatahadharisha kuhusu njama mpya za Marekani dhidi ya Yemen
Sep 02, 2023 07:33Mwanachama wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuhusu uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo na kusema kuwa, lengo la hatua hiyo ni kuandaa mazingira mapya na kufanya njama hatari na endelevu dhidi ya taifa la Yemen.
-
Mkuu wa Maulamaa wa Kisuni Iraq: Kambi ya Al-Houl inatumiwa na Marekani kuandaa magaidi wa DAESH (ISIS)
Sep 02, 2023 04:36Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Kisuni wa Iraq katika mkoa wa Diyala ametahadharisha juu ya hatari ya kambi ya al-Houl kwa usalama wa Iraq na eneo kwa ujumla na akaeleza kwamba kambi hiyo imeanzishwa na Marekani kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuandaa kizazi cha nne cha kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).
-
Velayati: Uanachama wa BRICS umevunja sera ya US ya kuitenga Iran
Aug 29, 2023 23:02Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kupewa uanachama Iran katika kundi la BRICS kumesambaratisha sera ya Marekani ya kujaribu kuitenga Jamhuri ya Kiislamu.