-
Russia: Mgogoro wa Syria yumkini ukageuka na kuwa mzozo kati ya Sunni na Shia
Apr 27, 2016 14:17Russia imeonya kuwa mgogoro unaoendelea kushuhudiwa hivi sasa nchini Syria huenda ukazusha mpasuko mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
-
Staffan de Mistura: Watu laki nne wameuawa katika vita nchini Syria
Apr 23, 2016 16:08Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria amesema watu wapatao laki nne wamepoteza maisha kutokana na vita vya zaidi ya miaka mitano vilivyoikumba nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani: Hakuna mpango wowote wa pili ghairi ya mazungumzo kwa ajili ya Syria
Apr 15, 2016 04:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Jared Caplan, amesema nchi hiyo haina mpango mwengine wowote wa pili kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria na kwamba mpango uliopo ni mmoja tu ambao ni mazungumzo.
-
Wananchi wa Syria wajitokeza kushiriki uchaguzi wa Bunge
Apr 13, 2016 07:16Wananchi wa Syria waliotimiza mashari ya kupiga kura wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura mapema leo, kushiriki uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo.
-
Rouhani na Putin: Wasyria watajiamulia mambo yao
Mar 28, 2016 14:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia juu ya udharura wa wananchi wa Syria kuachiwa wajiamulie mambo yao wenyewe.
-
Bashar al-Jaafari: Mashambulio ya Brussels ni matokeo ya sera ghalati za Magharibi kuhusiana na Syria
Mar 24, 2016 02:43Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa nchi hiyo katika mazungumzo ya Geneva amesema mashambulio ya kigaidi ya mjini Brussels, Ubelgiji ni matokeo ya siasa na sera ghalati za Magharibi kuhusiana na magaidi na mgogoro wa Syria.
-
Jordan yakataa kuwapa matibabu wakimbizi wa Syria
Mar 23, 2016 08:10Maelfu ya wakimbizi raia wa Syria wamenyimwa huduma muhimu za matibabu na nchi jirani ya Jordan.
-
Lavrov: Kuondoka vikosi vya Russia ni kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kutatua mgogoro wa Syria
Mar 16, 2016 07:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameeleza kuwa agizo lililotolewa na rais wa nchi hiyo la kutaka vikosi vya Russia kuondoka huko Syria halikutolewa ili kumfurahisha mtu, bali lengo la hatua hiyo ni kusaidia mchakato wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
-
UNICEF: Theluthi moja ya watoto wa Syria wamezaliwa kipindi cha vita
Mar 15, 2016 03:01Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia Watoto (UNICEF) umesema kila mtoto mmoja kati ya watatu nchini Syria amezaliwa katika kipindi cha vita,huku nchi hiyo ikiingia katika mwaka wa sita wa mapigano yaliyotokana na uasi unaoungwa mkono na madola ya kigeni.
-
Russia yapinga matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani
Mar 11, 2016 03:39Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amepinga vikali matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani dhidi ya Moscow akisema kuwa yanaweka hatarini mchakato wa kurejesha amani nchini Syria.