-
Askari wengine 144 wa Kenya wapelekwa Haiti kusaidia kurejesha usalama na utulivu nchini humo
Feb 07, 2025 07:23Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, amesema jukumu la kudhamini usalama linalotekelezwa na kikosi cha usaidizi cha mataifa kadhaa (MSS) kikiongozwa na nchi hiyo huko Haiti linazidi kuimarishwa na kupata nguvu zaidi ikiwa ni uthibitisho wa namna taifa hilo la mashariki ya Afrika linavyotimiza ahadi yake kwa Jamii ya Kimataifa.
-
Uasi ndani ya jela Msumbiji, wafungwa 33 wauawa, zaidi ya 1,500 watoroka
Dec 26, 2024 07:00Wafungwa wasiopungua 1,534 wametoroka katika jela moja iliyoko karibu na mji mkuu wa Msumbiji, Maputo katika tukio linalodaiwa kupangwa na kuhusishwa na maandamano ya machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba.
-
Marais wa Iran na Misri waonesha matumaini ya kustawi uhusiano wa pande mbili
Dec 20, 2024 10:04Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana mjini Cairo, Misri na wamepitia hatua zote chanya za kuweza kustawisha uhusiano kati ya nchi zao. Wameelezea matumaini yao kuwa hatua chanya zitaendelea hadi uhusiano wa nchi mbili utakaporejeshwa kikamilifu.
-
Rais Pezeshkian: Uhusiano mzuri baina ya nchi za Kiislamu utazima njama za maadui
Dec 19, 2024 00:13Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema "kadiri tutavyoweza kuboresha uhusiano wetu na nchi za Kiislamu ndivyo tutakavyoweza zaidi kuzima njama za maadui dhidi yetu".
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aelekea Misri kushiriki kikao cha D-8
Dec 17, 2024 23:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameelekea mjini Cairo Misri kwa ajili ya kushiriki kwenye kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la D-8 la nchi za Kiislamu zinazostawi.
-
Mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani Namibia: Hatutayakubali matokeo ya uchaguzi
Dec 01, 2024 02:43Mgombea mkuu wa urais wa upinzani nchini Namibia, Panduleni Itula, amesema chama chake hakitatambua matokeo ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa kuongezewa muda wa upigaji kura na kutawaliwa na fujo na madai ya uchakachuaji.
-
Mbunge wa UK: FIFA na UEFA zina 'nyuso mbili za ubaguzi wa rangi' kwa maslahi ya Israel
Nov 14, 2024 02:38Mbunge wa chama cha Leba nchini Uingereza Zarah Sultana amekosoa vikali mashirikisho ya juu ya soka duniani ya FIFA na UEFA kwa kutoziadhibu timu za soka za Israel wakati utawala huo wa Kizayuni unaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
UN: Nchi zinazohusika ziache kuzipatia silaha pande zinazopigana nchini Sudan
Nov 13, 2024 08:26Umoja wa Mataifa umesema, kuendelea kuwasambazia silaha askari wa jeshi na wa vikosi vya wanamgambo wanaopigana nchini Sudan ndiko "kunakowezesha kufanyika uchinjaji" na lazima kukomeshwe wakati raia wa nchi hiyo wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa vita.
-
Iran yaendelea na jitihada za kusimamishwa vita Ghaza na Lebanon
Oct 31, 2024 03:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Misri, Indonesia na Qatar na kujadiliana nao masuala ya kikanda na uhusiano wa pande mbili ikiwa ni muondelezo wa jitihada za Iran za kuhakikisha vita vinakomeshwa huko Ghaza na Lebanon.
-
Iran na Misri zataka Israel ilazimishwe kukomesha jinai zake Gaza, Lebanon
Oct 24, 2024 02:48Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian na mwenzake wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi wamesisitiza kuwa uchokozi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon ni lazima usitishwe, na kutoa wito wa kuwepo juhudi za kuzuia kuenea kwa mzozo katika maeneo mengine ya eneo la Asia Magharibi.