Pars Today
Askari 14 wa vikosi vya serikali ya mwafaka wa kitaifa ya Libya wameuliwa katika mashambulio ya anga yaliyofanywa na vikosi vinavyojiita Jeshi la Taifa la Libya vinavyoongozwa na Jenerali mstaafu Khalifa Haftar.
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema kuwa, maelfu ya wanajeshi wa nchi hiyo wameelekea katika mpaka wa Mexico kwa lengo la kile kilichotajwa kuwa ni kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo.
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram limedai kuwa wanachama wake wametekeleza shambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua askari 30 wa nchi hiyo.
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kinawazuilia askari wake watano wanaotuhumiwa kuuza kinyume cha sheria suhula na bidhaa za kikosi hicho.
Watu wenye silaha wamefanya shambulio katika eneo la kaskazini mwa Mali na kuua wanajeshi watatu wa nchi hiyo.