Jan 30, 2019 07:26 UTC
  • Maelfu ya wanajeshi wa Marekani waelekea katika mpaka wa Mexico

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema kuwa, maelfu ya wanajeshi wa nchi hiyo wameelekea katika mpaka wa Mexico kwa lengo la kile kilichotajwa kuwa ni kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo.

Patrick Shanahan amesema kuwa wanajeshi  wa Marekani wametumwa katika mpaka wa Mexico ili kuweka uzio wa nyaya za ziada na kuzidisha usimamizi katika eneo hilo la mpaka na Mexico. Hivi sasa pia karibu wanajeshi 2400 wa Marekani wametumwa katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico ili kusaidia kulinda usalama.  

Hitilafu zilizokuwa zimejitokeza kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na kongresi ya nchi hiyo kuhusu kupasisha bajeti ya kujenga ukuta wa mpakani huko Mexico zilisababisha kufungwa taasisi muhimu za serikali ya Marekani tangu Disemba 22 mwaka jana hadi Ijumaa ya tarehe 25 mwezi huu. Hatimaye Rais Trump na kongresi ya Marekani wamekubaliana kuidhinisha bajeti ya muda ili kuanza tena shughuli za serikali huku pande hizo zikiendelea kufanya mazungumzo kuhusu bajeti ya ujenzi wa ukuta huo wa mpakani. 

Tags