-
Takwa la Pakistan la kutofanya biashara ya mafuta na utawala wa Kizayuni
Aug 11, 2024 23:15Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Pakistan amelaani kuuawa shahidi Ismail Haniye aliyekuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kuelezea wasiwasi wake mkubwa alionao kuhusiana na chokochoko zinazoongezeka za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.
-
Pakistan yamtangaza rasmi Netanyahu kuwa ni gaidi, yaitaka Jamii ya Kimataifa nayo pia ifanye hivyo
Jul 23, 2024 03:02Serikali ya Pakistan imetangaza kuwa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni, ni "gaidi".
-
Azma ya Pakistan ya kuimarisha uhusiano wa pande zote na Iran
Jul 11, 2024 03:47Muhammad Shahbaz Sharf Waziri Mkuu wa Pakistan amesisitiza katika mazungumzo ya simu na Masoud Pezeshkian Rais Mteule wa Iran kuwa Islamabad iko tayari kustawisha uhusiano na Tehran. Waziri Mkuu wa Pakistan amesema kuwa mapatano yaliyofikiwa na nchi mbili katika ziara ya mwezi Aprili ya Rais Shahidi Raisi wa Iran huko Pakistan ni nukta muhimu katika uhusiano wa pande mbili.
-
Mokhber: Nchi za Waislamu ziungane kuzima jinai za Israel Gaza
Jun 17, 2024 04:16Kaimu Rais wa Iran ametaka kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa nchi za Waislamu ili kukomesha jinai na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Rais wa Iran asisitiza kukuza ushirikiano wa pande mbili na Pakistan
Apr 22, 2024 23:39Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kukuza ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad katika nyanja mbalimbali.
-
Rais wa Iran awasili Pakistan katika ziara ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na usalama
Apr 22, 2024 03:12Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad katika ziara rasmi ya kikazi yenye lengo la kuimarisha usalama na uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili.
-
Mvua kali za mafuriko zaua watu wasiopungua 168 Pakistan na Afghanistan
Apr 20, 2024 07:11Watu wasiopungua 168 wamepoteza maisha katika matukio yaliyosababishwa na mvua, baada ya mvua kali na mafuriko kuikumba Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan.
-
Uamuzi wa Pakistan dhidi ya harakati ya Zainabiyyun; malengo na matokeo yake
Apr 14, 2024 09:41Serikali ya Pakistan imechukua uamuzi wa kushtukiza na uliowashangaza na kuwapiga butwaa watu wengi, nao ni wa kuiweka harakati ya Zainabiyyun kwenye orodha yake ya tasisi za kigaidi licha ya kwamba harakati hiyo muda wote imekuwa ikipigania amani na usalama kwa Pakistan.
-
Watu wenye silaha waua abiria 11 kusini magharibi mwa Pakistan
Apr 13, 2024 23:00Watu wenye silaha wameua abiria wasiopungua 11 katika matukio mawili tofauti yaliyojiri kusini magharibi mwa Pakistan.
-
Raisi: Madola ya kibeberu yanazusha fitna ili kuvuruga usalama kati ya Iran na Pakistan
Apr 12, 2024 07:48Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan hakufurahishi madola ya kibeberu na kwa hivyo yanazusha fitna ili kuleta mpasuko kati ya mataifa hayo mawili na nchi hizo mbili za Kiislamu.