Apr 23, 2024 03:09 UTC
  • Rais wa Iran asisitiza kukuza ushirikiano wa pande mbili na Pakistan

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kukuza ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad katika nyanja mbalimbali.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema jana Jumatatu katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Muhammad Shahbaz Sharif Waziri Mkuu wa Pakistan huko Islamabad mji mkuu wa nchi hiyo kwamba: Uusiano kati ya Iran na Pakistan hauwezi kuvunjika. Raisi ameashiria pia kuwa nchi mbili za Iran na Pakistan zinapasa kupandisha juu uhusiano wao katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kiutamaduni. 

Rais Sayyid Ebrahim Raisi aliongeza kusema kuwa pande mbili za Iran Pakistan zina uwezo na suhula nyingi ambapo nchiimbili zinaweza kubadilishana na kutumia suhula hizo kwa maslahi ya nchi mbili na watu wake. 

Katika upande mwingine Rais wa Iran ameitaja misimamo ya pamoja  ya Iran na Pakistan katika vita dhidi ya ugaidi na kuongeza kuwa nchi mbili zimedhamiria pakubwa kupambana na machafuko na jinai iliyoratibiwa ya madawa ya kulevya na huu ni mtazamo wa pamoja wa nchi mbili za Iran na Pakistan. 

Katika mazungumzo hayo, naye Muhammad Shahbaz Sharif Waziri Mkuu wa Pakistan pia ameeleza kuwa Iran na Pakistan zina wasiwasi na mauaji ya kimbari ya watu wa Gaza na kuilani Israel. Amesema Tehran na Islamabad zinazitolea wito nchi mbalimbali duniani kukomesha haraka mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza haraka iwezekanavyo. 

 

Rais Rbrahim Raisi na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif 

Waziri Mkuu wa Pakistan aidha amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Iran hadi kuundwa nchi ya Palestina, mji wake mkuu ukiwa ni Quds.  

Tags