-
Haniya: Mapambano yataendelea mpaka Palestina iliyoanzia kwenye Mto hadi Baharini itakapokombolewa
Jun 25, 2022 21:52Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, mapambano na muqawama ungali unaongeza nguvu zake hadi ufike wakati wa kukombolewa Palestina iliyoanzia Mto Jordan hadi Bahari ya Mediterania.
-
Ismail Haniyeh: Jinai za utawala wa Kizayuni, hazitofautishi baina ya Waislamu na Wakristo
Jun 24, 2022 22:33Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel hautofautishi kati ya Waislamu na Wakristo katika jinai zake dhidi ya Palestina.
-
HAMAS: Israel iache kuchimba mashimo kwenye ua wa Msikiti wa Al-Aqsa
Jun 24, 2022 08:57Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeutaka utawala haramu wa Israel uache mara moja kitendo chake cha kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea katika msikiti mtatatifu wa al-Aqsa.
-
Wapalestina 3 wauawa shahidi na jeshi la Israel mjini Jenin
Jun 17, 2022 06:56Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi vijana watatu wa Kipalestina katika mji wa Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
HAMAS: Shambulio la Israel dhidi ya Syria linatokana na kufeli mpango wa kuanzisha uhusiano na Israel
Jun 13, 2022 03:30Mkuu wa Ofisi ya Mahusiano ya Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, shambulio la utawala haramu wa Israel dhidi ya Syria sababu yake ni kushindwa mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
-
Wanamuqawama wa Palestina Gaza wafanyia majaribio makombora yao
Jun 12, 2022 03:23Duru za kiusalama huko Palestina zimedokeza kuwa, vikosi vya muqawama vya nchi hiyo vimefanyia majaribio makombora yao katika fukwe za Ukanda wa Gaza.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kutapelekea kudhalilika madola ya Kiarabu
Jun 08, 2022 07:22Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema tawala za Kiarabu zilizokhitari kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel bila ridhaa ya wananchi wao hazitakumbwa na hatima nyingine ghairi ya kuishia kudhalilishwa na kutumiwa vibaya na utawala huo haramu.
-
UN: Israel kupora ardhi na kuwabagua Wapalestina, chachu ya ghasia na migogoro
Jun 08, 2022 06:23Timu ya ngazi ya juu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na kuwafanyia Wapalestina vitendo vya kibaguzi ndio sababu kuu ya kushuhudiwa mawimbi ya ghasia zisizokwisha katika ardhi hizo zilizoghusubiwa.
-
Abdollahian: Iran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina
Jun 06, 2022 23:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitoruhusu kukanyagwa haki za Wairani katika mazungumzo (ya Vienna) au kupuuza haki za wananchi Waislamu wa Palestina na kueleza bayana kuwa, Tehran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Wapalestina.
-
HAMAS: "Muqawama" ndiyo njia pakee ya kupambana na wavamizi na kuwashinda
Jun 06, 2022 22:01Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, njia pekee ya kuweza kupambana na kuwashinda wavamizi ni muqawama na mapambano ya kila upande, ya silaha, ya kisiasa, ya kijamii, ya kiuchumi na ya kidiplomasia.