Pars Today
Rais Ebrahim Raisi amesisitiza kuhusu misimamo ya wazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo vya kidhalimu lilivyowekewa taifa hili.
Mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana kati ya Iran na Marekani kuhusu uondoaji vikwazo yaliyoanza juzi Jumanne katika mji mkuu wa Qatar, Doha yamemalizika; huku pande mbili zikisema kuwa zitaendelea kuwasiliana juu ya marhala zijazo za mazungumzo hayo.
Kiongozi wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA anaelekea Doha, mji mkuu wa Qatar kwa ajili kushiriki duru mpya ya mazungumzo ya kuiondolea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu.
Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz amemuandikia barua Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani akiiomba Doha ichukue hatua za kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Riyadh.
Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani, Amir wa Qatar aliwasili mjini Tehran siku ya Alhamisi kwa ziara rasmi ambapo amekutana na kuzungumza na mwenyeji wake Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema dhulma ya miongo kadhaa ya utawala khabithi wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina ni ukweli mchungu wa historia na pigo kwa ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataraji kwamba ulimwengu wa Kiarabu utaingia wazi wazi katika medani ya kisiasa kukabiliana na jinai hizo.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imelaani vikali mpango mpya wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina.
Katika mazungumzo ya simu na Amir wa Qatar, Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu Iran amesisitiza utayarifu wa Iran katika kuisaidia nchi hiyo kuandaa kwa mafanikio Kombe la Dunia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio tatizo kuu la Ulimwengu wa Kiislamu.
Amir wa Qatar amekosoa vikali hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na kusisitiza kuwa, asilimia kubwa ya jamii ya kimataifa imefumbia macho kadhia hiyo kwa miongo kadhaa sasa.