-
Larijani: Hatua ya Trump dhidi ya Quds ni kujaribu kuficha kushindwa Marekani katika eneo hili
Dec 11, 2017 23:07Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Iran amesema kuwa, kitendo cha rais wa Marekani, Donald Trump cha kuitangaza Quds ambayo ina Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa Israel, ni kujaribu kuficha kufeli siasa za Marekani katika eneo hili.
-
Iran: Dunia imeungana kumlaani Donald Trump
Dec 11, 2017 11:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na masuala mengi tofauti ikiwemo ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza hapa mjini Tehran, suala la Quds, Yemen na masuala mengine mbalimbali.
-
Mogherini: Umoja wa Ulaya hautoitambua Quds kuwa ni mji mkuu wa Israel
Dec 11, 2017 11:13Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amepinga wito wa Tel Aviv wa kuutaka umoja huo kufuata mkono wa Marekani na kuutambua mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa Israel.
-
Wananchi wa Mauritania waandamana kumlaani Donald Trump
Dec 11, 2017 11:02Wananchi wa Mauritania wameungana na Waislamu na wapenda haki katika kona zote za dunia kuendeleza maandamano ya kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa hatua yake ya kuitambua Quds kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
-
Watawala vibaraka wa Kiarabu wabanwa; wananchi wataka viongozi wapya
Dec 11, 2017 09:39Malalamiko na maandamano ya wananchi wa nchi za Kiarabu si tu kwamba yamewalenga Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahi, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel pekee bali pia watawala vibaraka wa Kiarabu wanafanya eti mapatano ya amani na Wazayuni kwa madhara ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.
-
Hossein Amir-Abdollahian: Iran inakitetea kibla cha kwanza cha Waislamu
Dec 11, 2017 04:44Hossein Amir-Abdollahian, msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Iran daima imekuwa mtetezi wa haki za wananchi madhulumu wa Palestina na kibla cha kwanza cha Waislamu na itaendelea kufanya hivyo.
-
Kikao cha dharura cha nchi za Kiarabu kuhusu Quds Tukufu na maamuzi yaisyoweza kutekelezeka
Dec 11, 2017 04:28Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Jumamosi walikutana katika kikao cha dharura mjini Cairo Misri kujadili na kulaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kutambua Quds Tukufu (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais wa Iran: Uamuzi usio sahihi wa Trump ni sawa na kumwagia petroli kwenye moto
Dec 10, 2017 13:05Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uamuzi wa hivi karibuni wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuitangaza Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa Israel na kutoa amri ya kuhamishiwa ubalozi wa Washington katika mji huo ulikuwa sawa na kumwagia mafuta ya petroli katika moto katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Al Azhar yataka kufanyika mkutano wa kimataifa kujadili suala la Quds
Dec 10, 2017 10:57Sheikh Mkuu wa al Azhar ya Misri ametahadharisha kuhusu taathira za uamuzi wa Trump wa kuutambua rasmi mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kutaka kufanyika mkutano wa kimataifa wa kujadili suala hilo.
-
Somalia yasema hatua ya Trump dhidi ya Quds ni 'hatari'
Dec 10, 2017 00:10Somalia imejiunga na nchi nyingine za Afrika kulaani hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.