Al Azhar yataka kufanyika mkutano wa kimataifa kujadili suala la Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37429-al_azhar_yataka_kufanyika_mkutano_wa_kimataifa_kujadili_suala_la_quds
Sheikh Mkuu wa al Azhar ya Misri ametahadharisha kuhusu taathira za uamuzi wa Trump wa kuutambua rasmi mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kutaka kufanyika mkutano wa kimataifa wa kujadili suala hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2017 10:57 UTC
  • Al Azhar yataka kufanyika mkutano wa kimataifa kujadili suala la Quds

Sheikh Mkuu wa al Azhar ya Misri ametahadharisha kuhusu taathira za uamuzi wa Trump wa kuutambua rasmi mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kutaka kufanyika mkutano wa kimataifa wa kujadili suala hilo.

Sheikh Ahmad al Tayyib amesema kuwa uamuzi huo wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Quds unaamisha kukanyagwa haki za Wapalestina na Waarabu katika mji wa Quds na kupuuzwa matukufu ya Waislamu na Wakristo. Sheikh al Tayyib amewataka maulamaa wa ngazi za juu wa al Azhar kuitisha kikao cha dharura kuchunguza athari za uamuzi huo wa Trump.  

Ahmad al Tayyib amewataka maulamaa wa ngazi za juu wa al Azhar kufanya kikao cha dharura kujadili uamuzi huo wa Trump. Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 6 mwezi huu alitangaza kuwa Washington imeutambua rasmi mji wa Quds kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kwamba inauhamishia ubalozi wake katika mji huo licha ya hatua yake hiyo kupingwa vikali kieneo na kimataifa. Matamshi hayo ya Trump yameukasirisha sana Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu. Mji wa Baitul Muqaddas ambako kuna Msikiti wa al Aqsa ambacho ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyoweza kutenganishwa na Palestina. 

Msikiti wa al Aqsa ulioko Baitul Muqaddas