-
Wito wa Putin wa kuanzishwa jumuiya ya kulinda usalama katika Ghuba ya Uajemi
Oct 05, 2019 13:50Baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018, Washington iliazisha siasa za kuiwekea Iran mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi. Vikwazo vya kiuchumi visivyo na kifani na mashinikizo makubwa ya Washington yamepelekea kuongezeka mivutano baina ya nchi hizo mbili na baadhi ya matokeo ya hali hiyo ni kuongezeka mivutano katika Lango Bahari la Hormuz na Ghuba ya Uajemi.
-
Rais Rouhani: Nguvu za taifa la Iran zimeongezeka sana hivi sasa licha ya mashinikizo makubwa ya maadui
Oct 02, 2019 11:18Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia mashinikizo ya maadui dhidi ya taifa la Iran na kusisitiza kuwa, nafasi ya taifa kubwa la Iran imekuwa kubwa zaidi kuliko huko nyuma baada ya mwaka mmoja na nusu wa mashinikizo na vikwazo vya mfululizo vya kiuchumi vya maadui.
-
Rais Rouhani: Jamii ya Kimataifa inahitaji mashirikiano ya kiuchumi ya baina ya pande kadhaa na ya kikanda
Oct 02, 2019 04:36Rais Hassan Rouhani ameashriia vikwazo chungu nzima vinavyowekwa katika uhusiano wa kiuchumi baina ya nchi, ongezeko la kila uchao la umasikini, kukosekana usalama, uhajiri na kupungua ukuaji wa uchumi duniani na akasisitiza kwa kusema: Mfumo wa Kimataifa unahitaji mashirikiano ya kiuchumi ya baina ya pande kadhaa na ya kikanda.
-
Trump na ahadi zake bandia za kuiondolea Iran vikwazo baada ya kufanyika mazungumzo
Sep 30, 2019 12:06Baada ya kuiondoa nchi yake kwenye mapatano ya nyuklia mwezi Mei mwaka jana na kisha kuiwekea vikwazo vikali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika miezi ya hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha hamu kubwa ya kutaka kufanya mazungumzo na Iran ambapo baada ya kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kulienea fununu za uwezekano wa kukutana marais wa Iran na Marekani kando ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Zarif: Iwapo Marekani inataka mazungumzo na Iran lazima itekeleze ahadi zake
Sep 29, 2019 07:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran haitaacha mustakabali wa uchumi na wananchi wake utegemee mkutano wa kimaonyesho na Rais Donald Trump wa Marekani. Ameongeza kuwa, kama ambavyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alivyosema, 'iwapo Mareknai inataka kufanya mazungumzo na Iran, ni lazima kwanza itekeleze ahadi zake na isitishe vikwazo.'
-
Rouhani: Nchi za Ulaya zimekiri hazijui aliyeshambulia Aramco
Sep 28, 2019 02:40Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema licha ya nchi za Ulaya kuituhumu Tehran kuwa imehusika katika mashambulizi yaliyolenga kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia, lakini viongozi wa nchi hizo wamekiri wazi kuwa hawajui ni nani aliyetekeleza hujuma hizo.
-
Rouhani: Vikwazo vya kikatili vya Marekani vimeongeza mshikamano nchini Iran
Sep 26, 2019 12:32Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya kikatili vya Marekani dhidi ya Tehran vimeshindwa kufikia malengo yake, na badala yake vimeongeza mshikamano miongoni mwa wananchi wa Iran.
-
Muungano wa Matumaini, lugha ya amani katika kilele cha nguvu na uwezo
Sep 26, 2019 07:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiwa anawakilisha Wairani wote katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amezungumza kuhusu amani na 'Muungano wa Matumaini' na wakati huo huo akatoa kauli yenye nguvu na kutahadharisha kuhusu chokochoko zozote dhidi ya Iran.
-
Rais Rouhani akosoa kimya cha Umoja wa Mataifa kuhusu ugaidi wa kiuchumi Marekani dhidi ya Iran
Sep 26, 2019 04:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kukosoa kimya cha umoja huo mbele ya ugaidi wa kiuchumi wa serikali ya Marekani dhidi ya taifa la Iran.
-
Rais Rouhani: Katu hatutofanya mazungumzo na adui chini ya vikwazo
Sep 25, 2019 16:22Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni jambo lisiloyumkinika kwa taifa hili kufanya mazungumzo na adui likiwa chini ya mashinikizo na vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume cha sheria.