-
Russia: Kwa mtazamo wa mkuu wa UNICEF watoto wa Ghaza si muhimu kama wenzao wa Ukraine
Jan 25, 2025 06:12Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amemshutumu mkuu wa UNICEF kwa kuwapa kipaumbele watoto wa Ukraine kuliko watoto wenzao wa Ghaza baada ya kushindwa kulieleza Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu masaibu ya watoto hao kama alivyofanya kwa watoto wa Ukraine.
-
Pezeshkian: Iran na Russia hazitakubali kuburuzwa na maadui
Jan 25, 2025 03:03Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa, mapatano kamili ya ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Russia yanaonyesha kwamba Tehran na Moscow kamwe hazitakubali matakwa ya kupindukia ya maadui, akisisitiza kuwa nchi mbili hizi zitashirikiana kuunda sera zinazotoa kipaumbele kwa masuala ya utulivu, usalama, maendeleo na ustawi wa uchumi katika eneo.
-
Kutekelezwa Makubaliano ya Kifedha kati ya Iran na Russia
Jan 21, 2025 02:33Gavana wa Benki Kuu ya Iran, Mohammadreza Farzin, amesema kuwa kupitia utekelezaji wa makubaliano ya kifedha kati ya Iran na Russia, sarafu za mataifa haya mawili zitakuwa msingi wa biashara kati ya nchi hizo kwa mujibu wa kiwango cha mabadilishano kilichokubaliwa sokoni.
-
Araqchi: Asili ya makubaliano ya Iran na Russia ni ya kiuchumi
Jan 18, 2025 11:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya kina ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Iran na Russia yanahusu vipengee vyote vya uhusiano wa nchi na kwamba asili ya makubaliano hayo zaidi ni katika uga wa uchumi.
-
Russia yasisitiza umuhimu wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kistratejia na Iran
Jan 16, 2025 04:28Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin (makao makuu ya urais wa Russia), Jumanne alisema kuwa Russia inatilia umuhimu mkubwa kusainiwa mkataba wa ushirikiano wa kina wa kistratejia na Iran, akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu muhimu sana ya safari ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
-
Maana ya ushirikiano mpya wa Iran na Russia kwa ulimwengu
Jan 10, 2025 12:44Chombo kimoja cha habari cha Russia kimetathmini ushirikiano wa Iran na Russia na kuandika: Makubaliano ya pamoja ya kistratejia ni hatua muhimu katika kuimarika muungano kati ya mataifa haya mawili.
-
Vikwazo vipya vya Washington dhidi ya Iran na Russia kwa kisingizio cha kuingilia uchaguzi wa Marekani
Jan 02, 2025 12:16Wizara ya Hazina ya Marekani ilitangaza katika taarifa yake Jumanne iliyopita kuwa: "Idara ya Udhibiti wa Mali za Kigeni (OFAC) imeiwekea vikwazo taasisi tanzu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) na shirika tanzu la Idara ya Ujasusi ya Russia (GRU) yenye makao yake makuu mjini Moscow na mkurugenzi wake.
-
Intelijensia ya Russia: US na UK zinapanga mashambulio ya kigaidi dhidi ya vituo vyetu vilivyoko Syria
Dec 29, 2024 11:03Idara ya Intelijensia ya Russia ya Nje ya Nchi (SVR) imetahadharisha kuwa Marekani na Uingereza zinapanga mashambulizi ya kigaidi katika vituo ya kijeshi vya nchi hiyo vilivyoko Syria ili hali ya nchi hiyo isitangamae na amani na uthabiti usirejee nchini humo.
-
Waasi wa ADF waua raia wasiopungua 21 mashariki ya DRC katika wiki ya Krismasi
Dec 29, 2024 11:01Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) wameua watu wasiopungua 21 katika mashambulio kadhaa waliyofanya katika wiki ya Krismasi kwenye eneo lililokumbwa na mgogoro wa vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Baada ya Israel kuichoma moto hospitali kuu ya kaskazini ya Ghaza, yamkamata mkurugenzi na wafanyakazi wake
Dec 28, 2024 14:12Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa askari wa jeshi la utawala w Kizayuni wa Israel wamemkamata Hussam Abu Safiya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Ghaza, na wafanyakazi wengine mapema leo, siku moja baada ya askari wa jeshi hilo kuichoma moto hospitali hiyo, ambayo ndicho kituo kikuu pekee cha afya katika eneo hilo.