-
Ramaphosa: NATO ndiyo ya kulaumiwa kwa vita vya Russia nchini Ukraine
Mar 18, 2022 11:31Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameilaumu NATO kwa vita vya Ukraine na kusema kuwa atapinga wito wa kuilaani Russia. Matamshi haya ya Ramaphosa yanatia shaka iwapo atakubaliwa na Ukraine au nchi za Magharibi kama mpatanishi katika mzozo huo.
-
Mkurugenzi Mkuu wa WHO: Migogoro yote duniani inapasa ipewe umuhimu
Mar 18, 2022 04:07Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema, wakati macho yote yameelekezwa kwenye mgogoro wa Ukraine, zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Afghanistan wanahitaji msaada.
-
Russia yaangamiza mifumo 11 ya ulinzi wa makombora ya jeshi la Ukraine
Mar 17, 2022 19:03Wizara ya Ulinzi ya Russia imetoa taarifa ikibainisha kuhusu mchakato wa mashambulizi ya nchi hiyo huko Ukraine na kutangaza kuwa, katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita imeangamiza ndege mbili za kivita, droni 12 na ghala moja la kijeshi la Ukraine.
-
Vituo vya Kiislamu vya Russia vyalaani mashambulizi ya kipropaganda ya Magharibi dhidi ya nchi hiyo
Mar 17, 2022 05:21Vituo vya Kiislamu vya Russia vimelaani propaganda za chuki za nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na ubaguzi dhidi ya raia wa Russia.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Russia na matokeo yake
Mar 17, 2022 03:08Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili mjini Moscow siku ya Jumanne akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Sergey Lavrov, Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Russia kuhusu masuala ya pande mbili, mazungumzo ya Vienna, Ukraine, Syria, Yemen na Afghanistan.
-
Lavrov: Kwa hakikisho la maandishi la US, vikwazo vya Magharibi havitaathiri ushirikiano wa Russia na Iran
Mar 15, 2022 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya nchi yake kwa kisingizio cha vita vya Ukraine havitaathiri ushirikiano wa Moscow na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Amir-Abdollahian: Kustawisha uhusiano na Russia kuna umuhimu kwa Iran
Mar 15, 2022 10:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, bila kujali matukio na mabadiliko yoyote yanayojiri kimataifa, kustawisha uhusiano na Russia kuna umuhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Macron na Biden waafikiana kuongeza vikwazo dhidi ya Russia
Mar 14, 2022 04:43Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani kuhusu mashambulio ya Russia dhidi ya Ukraine, na pande hizo mbili zimekubaliana kuzidisha vikwazo dhidi ya Moscow.
-
Kukiri EU kosa lake la kuiahidi Ukraine kujiunga na NATO
Mar 13, 2022 23:23Josep Borrell Fontelles, Mkuu wa Sera za Kigeni za Umoja wa Ulaya amekiri kuwa kitendo cha umoja huo cha kuipa ahadi Ukraine ya kuiunga na Jeshi la Nchi za Magharibi NATO, lilikuwa kosa.
-
Russia: Marekani na washirika wake wanaunda silaha za kibaolojia nchini Ukraine
Mar 12, 2022 22:49Russia imekutaja kuwepo kwa shughuli za kibaolojia nchini Ukraine kuwa ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa na kutangaza kuwa, ina nyaraka zinazothibitisha kuwepo kwa maabara 30 za kibaolojia zenye kemikali za vimelea vinavyosababisha magonjwa hatari kama tauni na kimeta kupitia ndege wanaohama kati ya Ukraine na Russia.