-
Merkel: Ulaya huru inapaswa kupunguza mivutano kati yake na Russia
Jun 26, 2021 02:46Kansela wa Ujerumani amesema kuwa, Umoja wa Ulaya wenye nguvu za kiutawala na uhuru, unabidi ulinde manufaa ya nchi za bara hilo na ufanye mazungumzo na Russia kama yale yaliyofanyika baina ya rais wa Marekani, Joe Biden na Rais Vladimir Putin wa Russia.
-
Jenerali Gerasimov: Russia inalinda haki yake ya kutumia silaha za nyuklia kujibu mapigo
Jun 24, 2021 22:59Kamanda wa Majeshi ya Russia amesema kuwa Moscow inalinda haki yake ya kutumia silaha za nyuklia kwa ajili ya kujibu mashambulizi ya mabomu ya nyuklia au silaha nyingine za mauajii ya umati dhidi ya nchi hiyo na waitifaki wake.
-
Russia: Mazungumzo ya JCPOA yamefika marhala ya mwisho
Jun 24, 2021 02:47Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na ambaye pia ni afisa wa ngazi ya juu katika timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Russia ametangaza kuwa, mazungumzo ya kuhuisha mapatano ya JCPOA yamefikia marhala ya mwisho.
-
Russia yaanza mazoezi ya kijeshi eneo ambako Marekani pia inapanga mazoezi ya kivita
Jun 11, 2021 07:53Jeshi la Majini la Russia limeanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la kati mwa Bahari ya Pasifiki punde baada ya Marekani kusema itafanya mazoezi makubwa zaidi ya kivita katika eneo hilo hilo katika msimu wa joto mwaka huu.
-
Rouhani: Iran inaunda vituo 2 vya nishati ya nyuklia kwa ushirikiano na Russia
Jun 10, 2021 08:21Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imeanza ujenzi wa vinu viwili vipya vya nishati ya nyuklia kwa ushirikiano na Russia.
-
Russia: Wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni wavamizi, waondoke
Jun 09, 2021 07:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wanajeshi wa Marekani ni wavamizi nchini Syria na wako huko kinyume cha sheria, hivyo wanapaswa waondoke.
-
Rais Putin wa Russia naye atabiri kuwa Marekani inaelekea kusambaratika
Jun 07, 2021 08:53Rais Vladimir Putin wa Russia katika kikao chake cha hivi karibuni na waandishi habari pembizoni mwa Kongamano la Kimataifa la Uchumi mjini St. Petersburg alisema kuwa Marekani inakumbwa na matatizo ambayo madola makubwa hukumbana nayo. Amebaini kuwa matatizo ambayo Marekani inakabiliana nayo yanatokana na nguvu ilizonazo na sasa imeshindwa kutatua matatizo hayo na hali hiyo ndiyo ile ile liliyokumbana nayo Shirikisho la Sovieti.
-
Iran, China na Russia zashauriana kuhusu mazungumzo yajayo ya JCPOA
May 31, 2021 22:22Mwakilishi wa Russsia katika taasisi za kimataifa zenye makao mjini Vienna nchini Austria amesema kuwa jumbe za Iran, China na Russia zimejadiliana huko Vienna kuhusu hatua mazungumzo yajayo ya JCPOA.
-
Putin ataka mashambulio ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina yasimamishwe mara moja
May 18, 2021 09:20Rais Vladimir Putin wa Russia ametaka mashambulio ya kinyama yanayotekelezwa na utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya Wapalestina yasimamishwe mara moja.
-
Ndege ya kijeshi ya Russia yatimua ndege ya kijasusi ya Marekani
May 06, 2021 08:07Russia imetangaza leo Alkhamisi kuwa imetumia ndege yake ya kivita kufukuza ndege ya kijasusi ya Marekani iliyokuwa ikijaribu kuingia katika anga ya nchi hiyo kinyume cha sheria katika Bahari ya Chukchi.