Kremlin: Uchokozi mwingine wa Uingereza utapewa jibu la kuangamiza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i72022-kremlin_uchokozi_mwingine_wa_uingereza_utapewa_jibu_la_kuangamiza
Msemaji wa Rais wa Russia amesema kuwa, hatua nyingine yoyote ya kichochezi kama ile iliyofanywa na manowari ya kivita ya Uingereza ya kuingia kinyume cha sheria katika maji ya nchi hiyo, itapewa jibu kali na la kuangamiza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2021 05:21 UTC
  • Dmitry Peskov
    Dmitry Peskov

Msemaji wa Rais wa Russia amesema kuwa, hatua nyingine yoyote ya kichochezi kama ile iliyofanywa na manowari ya kivita ya Uingereza ya kuingia kinyume cha sheria katika maji ya nchi hiyo, itapewa jibu kali na la kuangamiza.

Dmitry Peskov amesema, tukio hilo lilikuwa hatua ya kichochezi ililofanyika kwa mpangilio maalumu na kuongeza kuwa: Rais Vladimir Putin ameonesha kwamba, kukaririwa kitendo hicho kukakabiliwa na jibu kali la Moscow. 

Peskov amesema kuwa, jibu la Russia litakuwa kali na la kuangamia, na kwamba Washington na London zilishirikiana katika uchokozi huo. 

Awali msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Russia, Maria Zakharova alikuwa amesema hana shaka yoyote kwamba, kitendo hicho cha jeshi la Uingereza kilifanyika kwa mwafaka wa Marekani. 

Jumatano iliyopita manowari ya jeshi la Uingereza ya HMS Defender iliingia kinyume cha sheria katika maji ya Russia kwenye Bahari Nyeusi na kutahadharishwa kwa kivyatuliwa risasi na makombora na ndege za kivita za Russia. 

Tangu mwaka 2014 wakati Russia ilipoliunganisha eneo la Cremia na ardhi ya nchi hiyo baada ya kura ya maoni iliyofanyika eneo hilo, Washington na nchi za Magharibi kwa ujumla ziliiwekea vikwazo serikali ya Moscow kwa kisingizio eti cha kuzusha machafuko mashariki mwa Ukraine. Russia imekanusha madai hayo.