-
Kuendelea mashambulizi ya Saudi Arabia Yemen; raia watano wauawa mkoani Ta'iz
Feb 20, 2018 23:41Raia watano jana usiku waliuawa katika mashambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Saudia katika mkoa wa Taiz Yemen.
-
Ndege za kivita za Saudia zaua watu 18, wakiwemo watoto na wanawake, nchini Yemen
Feb 18, 2018 04:16Ndege za kivita za Saudi Arabia zimedondosha mabomu nchini Yemen na kuua watu 18, wakiwemo wanawake na watoto katika mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
-
Qassemi: Al Jubeir anabwabwaja, anataka kuzungumza kwa niaba ya Wairaqi
Feb 15, 2018 12:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu madai yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia katika kikao cha kuijenga upya Iraq dhidi ya Iran na kusema: Adel al-Jubeir amesahau kwamba hawezi kuzungumza kwa niaba ya serikali ya Iraq na wananchi wa nchi hiyo.
-
Makumi ya wanamgambo wa serikali za Sudan na Saudia wauawa nchini Yemen
Feb 15, 2018 00:34Duru mbalimbali za Yemen zimetangaza habari ya kuuawa makumi ya wanamgambo wa serikali za Sudan na Saudi Arabia katika vita na jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi ndani ya ardhi ya Yemen.
-
Uhusiano wa Saudia na Lebanon na kuzidi kupanda joto la mvutano baina ya pande mbili
Feb 10, 2018 02:36Kuna kila ishara inayoonyesha kuwa uhusiano wa Saudi Arabia na Lebanon unaelekea kwenye mkondo unaoshadidisha mvutano baina ya pande mbili.
-
Mwanaharakati wa kike aliyekosoa mahusiano ya Saudia na Israel aendelea kushikiliwa Riyadh
Feb 08, 2018 10:54Mwanaharakati wa kike ambaye alikosoa kitendo cha kuanzishwa mahusiano kati ya nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saudia, na utawala haramu wa Israel, anaendelea kushikiliwa katika korokoro za kutisha za utawala wa Aal Saud.
-
Utawala wa Aal Saud watwaa kwa siri kisiwa cha Tiran cha Misri
Feb 06, 2018 23:05Licha ya kuwepo malalamiko ya Wamisri wanaopinga utawala wa Aal-Saud kuuziwa visiwa viwili vya Tiran na Sanafir mali ya nchi hiyo, duru za habari zimearifu kwamba Saudia imetwaa kisiwa cha Tiran kilichopo Bahari Nyekundu kwa siri.
-
Maandamano London ya kupinga kuuziwa silaha Riyadh
Feb 05, 2018 04:23Makumi ya watu juzi waliandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini London Uingereza wakipinga na kulalamikia hatua ya Uingereza ya kuiuzia silaha Saudia.
-
Safari na Bin Salman Uingereza yaahirishwa kwa tuhuma za kufanya jinai dhidi ya binadamu
Feb 03, 2018 12:05Safari iliyopangwa kufanywa na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia nchini Uingereza imeahirishwa kwa muda usiojulikana baada wabunge, jumuiya za kiraia na makundi ya kutetea haki za binadamu kupinga safari hiyo.
-
Mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel ashangaa kutoshtakiwa Bin Salman na Al Nahyan
Feb 03, 2018 04:50Bi Tawakkol Karman, mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel wa nchini Yemen amesisitizia umuhimu wa kushtakiwa kimataifa Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme nchini Saudia na Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Abu Dhabi kutokana na jinai zao za mauaji ya umati nchini Yemen.