Amnesty International yaikosoa Ufaransa kwa kuziuzia silaha Imarati na Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40719-amnesty_international_yaikosoa_ufaransa_kwa_kuziuzia_silaha_imarati_na_saudi_arabia
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeikosoa vikali Paris kwa kuendelea kuiuzia Riyadh silaha na zana za kijeshi ambazo zinatumika vitani huko Yemen.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Feb 22, 2018 04:47 UTC
  • Amnesty International yaikosoa Ufaransa kwa kuziuzia silaha Imarati na Saudi Arabia

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeikosoa vikali Paris kwa kuendelea kuiuzia Riyadh silaha na zana za kijeshi ambazo zinatumika vitani huko Yemen.

Shirika la Amnesty International jana usiku lilitoa taarifa likiitaka Ufaransa kuacha kuziuzia silaha Saudi Arabia na Imarati kufuatia  nchi mbili  hizo kutenda jinai za kivita. Shirika hilo limeongeza kuwa raia wa Yemen wamagharamika pakubwa kutokana na kujiri vita vikubwa nchini kwao na kuzitaja pande zinazozozana huko Yemen kuwa wahusika wa matukio hayo yote. 

Vikosi vamizi vya Saudia katika uvamizi wao wa kijeshi huko Yemen 

Tarehe Nne mwezi Novemba mwaka 2015 Saudi Arabia na Ufaransa zilisaini makubaliano ya kuuziana silaha yenye thamani ya yuro bilioni mbili na milioni mia nane. Makundi ya kutetea haki za binadamu yameikosoa vikali serikali ya Ufaransa kwa hatua yake ya kuuzia silaha muungano vamizi wa Kiarabu huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia.  

Mwezi mmoja uliopita pia Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch alizitaka Marekani, Uingereza na Ufaransa ziache kuiuzia silaha Saudi Arabia. Kenneth Roth alieleza kuwa wakati umefika sasa kwa Marekani, Uingereza na Ufaransa kuacha kuiuzia silaha Saudia. Alibainisha kuwa silaha hizo zinatumiwa kuipiga Yemen na kuwasababishia maafa makubwa raia wa nchi hiyo wasio na hatia.