-
Wanajeshi wa Saudia waendeleza hujuma katika mji wa Al Awamiyah
May 24, 2017 23:56Baada ya kupita wiki mbili tokea wanajeshi wa Saudi Arabia wavamie mtaa wa Al Masourah mjini Al-Awamiya mashariki mwa nchi hiyo hali inaripotiwa kuwa mbaya huku ukandamizaji ukiendelea.
-
Iran: Mauaji ya waandamanaji Bahrain, matokeo ya awali ya safari ya Trump Riyadh
May 23, 2017 23:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushambuliwa na kuuawa wananchi wa Bahrain waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani ni matokeo ya kwanza ya safari ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump nchini Saudi Arabia.
-
Waislamu Pakistan: Mkutano wa Riyadh na Trump ulikuwa wa kupanga njama chafu dhidi ya Uislamu
May 23, 2017 10:52Kiongozi wa Jumuiya ya 'Ahlu Hurm' ya nchini Pakistan amekosoa vikali safari ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Saudia na kikao cha hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh, na kusema kuwa kikao hicho kimebainisha wazi kwamba baadhi ya nchi hazifungamani na mafundisho ya dini ya Uislamu, bali zinafungamana na dini ambayo msemaji wake ni Rais Trump.
-
Saudia mnunuzi mkubwa zaidi wa silaha za Marekani, Israel mpokezi mkubwa zaidi wa misaada ya kijeshi ya Marekani
May 23, 2017 02:33Utawala wa Kizayuni wa Israel umebainisha wasiwasi wake kuhusu Marekani kuiuzia Saudi Arabia silaha zenye kugharimu mabilioni ya dola katika hali ambayo Israel yenyewe inapokea misaada ya silaha za kisasa zaidi kutoka Marekani.
-
Independent: Hotuba ya Trump Saudia imetoa baraka kwa tawala za kidikteta Mashariki ya Kati
May 22, 2017 11:58Gazeti la The Independent linalochapishwa London, Uingereza limeandika kuwa hotuba iliyotolewa na Rais wa Marekani mjini Riyadh, Saudi Arabia ilikuwa sawa na ujumbe wa kutoa baraka kwa tawala za kiimla na kidikteta za Mashariki ya Kati (Magharibi ya Asia) za kuendeleza utesaji na ukandamizaji dhidi ya jamii za wachache katika nchi zao.
-
Afghanistan: Saudia na Qatar, ndio wafadhili wakuu wa genge la Daesh nchini mwetu
May 22, 2017 11:18Mjumbe wa Bunge la Afghanistan amesema kuwa, kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) linaendelesha harakati zake kaskazini mwa nchi hiyo kupitia uungaji mkono wa kifedha wa Saudia na Qatar.
-
Seneta wa US akosoa mauzo ya silaha kwa Saudia kwa dola bilioni 110
May 21, 2017 23:32Seneta mmoja wa chama cha Democratic nchini Marekani amekosoa vikali hatua ya Washington kusaini makubaliano ya mauzo ya silaha yenye thamani ya dola bilioni 110 za Marekani kwa Saudi Arabia, licha ya kufahamu fika kuwa silaha hizo zinatumiwa na watawala Riyadh kuwaua raia wa Yemen.
-
Human Rights Watch yamuonya Trump kuhusu kuiuzia silaha Saudia
May 21, 2017 23:27Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limemuona Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na kuiuzia silaha Saudi Arabia kutokana na nchi hiyo kutenda jinai dhidi ya wananchi wa Yemen.
-
Hizbullah: Safari ya Trump Saudia ni ya kiwendawazimu
May 21, 2017 09:35Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imeitaja safari ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Saudi Arabia kama ya kiwendawazimu na ambayo haitakuwa na tija yoyote kwa ulimwengu wa Kiislamu.
-
Iran: Lengo la Marekani ni kuudhoofisha ulimwengu wa Kiislamu
May 21, 2017 03:26Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa ya Bunge la Iran amesema, lengo la Marekani ni kuudhoofisha ulimwengu wa Kiislamu, kushadidisha mizozo katika eneo hili, kuuza silaha nyingi zaidi na kuweka kambi nyingi zaidi za kijeshi katika nchi kama vile Saudi Arabia.